GET /api/v0.1/hansard/entries/1128699/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1128699,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1128699/?format=api",
"text_counter": 94,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kamukunji, JP",
"speaker_title": "Hon. Yusuf Hassan",
"speaker": {
"id": 398,
"legal_name": "Yusuf Hassan Abdi",
"slug": "yusuf-hassan-abdi"
},
"content": " Tukifahamu kuwa nchi ya Tanzania iliunda Baraza la Kiswahili la Kitaifa (BAKITA) katika mwaka wa1967, na pia Zanzibar ikabuni Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA) katika mwaka wa 2004 kwa madhumuni ya kukuza na kuimarisha na kuendeleza mbele lugha ya Kiswahili katika Tanzania Bara pamoja na viziwa vya Zanzibar; tukitambua kwamba mukutano wa tatu wa Baraza la Mawaziri wa Kenya uliofanyika Tarehe 14 Agosti, 2018, uliidhinisha kuanzishwa kwa Baraza kuu la Kiswahili la Kitaifa kuambatana na Kifungo cha 137 cha Mkataba wa Uanzilishi wa Jumuia ya Afrika Mashariki; ikifahamika kwamba Kiswahili ni lugha ya kiaasili kwa jamii za eneo la Pwani nchini Kenya na pia idadi kubwa ya Wakenya ni wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili; tukijua kwamba lugha ya Kingereza ina nguvu sana katika mawasiliano rasmi na kwa hivyo kuchangia kuthoofika kwa lugha yetu ya Kiswahili; tukitambua uamuzi wa Baraza la Mawaziri kuhusu kubuniwa kwa halmashauri kuu ya Kiswahili ya kitaifa bado haujatekelezwa, kwamba Bunge hili linahimiza Serikali kuu, kupitia Wizara ya Michezo, Utamaduni na Uridhi, kuanzisha rasmi Baraza kuu la Kitaifa na kuzindua mikakati, mbinu na sera mahususi zinazohitajika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili na kushirikiana The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}