GET /api/v0.1/hansard/entries/1128853/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1128853,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1128853/?format=api",
"text_counter": 248,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": " Moja lilikuwa Swali na lingine Kauli . Yakawa mambo ni mawili katika moja. Jambo la kwanza linahusu nyongeza ya mishahara. Pili, kulikuwa na vijana 247. Wanakamati walioko hapa watakubaliana na mimi kuwa vijana chipukizi waliajiriwa lakini baada ya kila miezi michache wanaambiwa waendeni nyumbani wataregea. Licha ya kwamba KPA ilivunja sheria, kwa sababu sheria ya Kenya haikubali mpangilio huo; wasimamizi wakakubali kuwa wataelezea washaajiri watu wangapi tangu siku hiyo. Sasa ninaomba mwelekeo kwa sababu kuna taarifa ya kwamba wametangaza nafasi za kazi mia mbili. Waziri alitoa notisi kwamba ifikapo Novemba, Kamati itapatiwa jawabu kuhusu wale wafanyikazi 247 na kujulishwa ni lini wataregeshwa kazini. Sasa kwa vile KPA imetoa ilani ya kuajiri watu 200, tunaomba jambo hilo liangaziwe. Jambo la pili linahusu Kamati inayohusika na fedha. Tuliuliza swali tarehe 14 Octoba, 2021. Kwenye Swali hilo tumelalama kwamba halmashauri ya ushuru nchini (KRA) inalazimisha watu ambao PIN za kampuni zao ni za mji wa Mombasa kuchukua mizigo yao Nairobi. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Gladys Wanga, jana alithibitisha kwamba Wizara imeandikiwa barua lakini hawajaleta jawabu mpaka sasa. Kwa nini wafanyibiashara walioko Mombasa wanaangaliwa na macho tofauti kama kwamba sio Wakenya? Kwa hayo mambo mawili, tunaomba tusitiwe kiungulia. Tunataka masuala ya mji wetu na watu wetu wafaidike na chao. Nikizumgumza hapa sisemi ukabila, bali ni uzalendo. Tukisema mwana Mombasa na mpwani tunazungumzia mtu ambaye rasilimali yake iko pale, amezaliwa pale, anaishi na yuko na biashara katika eneo lile bila ya kujali rangi, dini wala kabila lake. Tunaenda katika likizo ambayo itakuwa ndefu. Ninaomba utoe mwelekeo ili haya Maswali yaweze kujibiwa wiki inayokuja. Hatutaki kuchukulia jiji la Mombasa kama kwamba gavana aliyeko ni gofu."
}