GET /api/v0.1/hansard/entries/1128860/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1128860,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1128860/?format=api",
"text_counter": 255,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mwea, JP",
"speaker_title": "Hon. Josphat Kabinga",
"speaker": {
"id": 13441,
"legal_name": "Josphat Kabinga Wachira",
"slug": "josphat-kabinga-wachira-2"
},
"content": "wakatuahidi kwamba watatupatia jawabu. Tangu wakati ule, tumekuwa tukimuuliza Waziri husika lakini hatujapata jawabu kuhusu hao wafanyikazi 247. Inasikitisha kwamba KPA wanataka kuajiri watu wengine kabla ya kutupatia jawabu. Nitachukua jukumu hili na kuwasiliana kupitia Ofisi ya Kiranja wa Bunge ili tuone kama tutamlazimisha Waziri kuleta jawabu wiki ijayo kwa sababu hili swali limekaa sana. Tutajaribu kuona kwamba jawabu limeletwa wiki ijayo. Pia, ningependa kutoa pole zangu kwa mwenzangu kwa sababu amekuwa akifuatilia jambo kwa makini. Ni vizuri kuona ya kwamba kuna wawakilishi katika Bunge hili ambao wanafuatilia masuala kama haya ndiyo maslahi ya watu wao yaweze kuzingatiwa vilivyo. Ninampongeza mwenzangu kwa sababu kila tunapokutana kwenye korido za Majengo ya Bunge, yeye huniuliza nimefikia wapi kuhusu swali hili. Ninamhakikishia kwamba nitafuatilia jambo hili mpaka tupate jawabu. Asante."
}