GET /api/v0.1/hansard/entries/1128864/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1128864,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1128864/?format=api",
"text_counter": 259,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nominated, JP",
"speaker_title": "Hon. David ole Sankok",
"speaker": {
"id": 13166,
"legal_name": "David Ole Sankok",
"slug": "david-ole-sankok"
},
"content": " Mhe. Naibu Spika wa Muda, mimi pia nilimuuliza Swali Waziri wa Masuala ya Ndani miezi mitatu iliyopita na bado sijapata jibu. Waziri alikuja katika Majengo ya Bunge na amerikodiwa kwenye Hansard akisema kwamba Naibu wa Rais ako na hectare 15,000 za ardhi kule Laikipia. Waziri alitoa stakabadhi ambazo zinaonyesha kwamba Naibu wa Rais ako na hiyo shamba kule Laikipia. Naye Naibu wa Rais akasema yeye hana shamba kule Laikipia. Sote tunajua kwamba kumekuwa na shida kule Laikipia, na watu wanauwana. Kwa hivyo, tuliona ni kana kwamba Waziri alikuwa analeta uzushi ili watu wa Laikipia waendelee kupigana. Vile vile, tuliona kamba Waziri alikuwa anawachochea watu ili wamchukie Naibu wa Rais. Kwa hivyo, tukamuuliza Swali alete cheti miliki cha ardhi hiyo tupate kuthibitisha iwapo kweli ile ardhi ni ya Naibu wa Rais. Naibu wa Rais alisema kama kuna shamba lake kule Laikipia, lipatiwe wananchi wenye tajriba ya chini. Pia, tulikuwa tunataka kujua iwapo shamba hiyo imegawanyiwa wananchi ambao wako kule Laikipia. Nimeitwa kutoka Narok mara tatu nikaja Bungeni ili nijibiwe lakini sijapata jawabu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}