GET /api/v0.1/hansard/entries/1128865/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1128865,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1128865/?format=api",
    "text_counter": 260,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nominated, JP",
    "speaker_title": "Hon. David ole Sankok",
    "speaker": {
        "id": 13166,
        "legal_name": "David Ole Sankok",
        "slug": "david-ole-sankok"
    },
    "content": "Mhe. Spika Justin Muturi alitoa mwelekeo kwamba nijibiwe hilo swali Alhamisi. Siku hiyo tukaja kwenye Chumba hiki lakini Waziri hakuja. Alituma naibu wake, ambaye alijibu Maswali mengine yote na kusema kwamba Swali langu kuhusu shamba ya hectare 15,000 waliyodai kuwa ya Naibu wa Rais hakuwa na jawabu. Kwa hivyo, ninakuomba kwa hekima yako uambie Kamati hiyo wamwambie Waziri anipatie nakala ya jawabu alilotayarisha ama aseme kwa mdomo niletewe jawabu ili niwapelekee watu wa Laikipia. Vilevile, tunataka kujua iwapo haya mambo yote yanayosemwa kuhusu Naibu wa Rais ni ya kuwekelewa na ya uongo . Asante sana."
}