GET /api/v0.1/hansard/entries/1129250/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1129250,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1129250/?format=api",
    "text_counter": 46,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Shukran sana kwa kunipatia nafasi ili nichangie Hotuba Rais alitoa kwa Taifa kuhusu maendeleo ambayo Serikali yake imefanya kufikia hivi sasa na yale matarajio ambayo anafikiria anaweza kuyafanya kwa hii miezi tisa au kumi iliyobaki kama Rais wa Jamhuri ya Kenya. Hatuwezi kusema kwamba asilimia, Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Muigai Kenyatta amefaulu. Hapana! Yeye kama kiongozi wa kisiasa pia ana makosa yake. Kuna pia unyonge wake mahali fulani. Kwa hivyo, tunasema kwamba alijaribu na hivi sasa amejaribu na atajaribu. Mengine yatakuwa mazuri na mengine hayatafaa. Jambo la kwanza ambalo ningependa kuongea juu yake ni kwamba katika Hotuba ya Rais, ni vyema aliongea habari ya Lamu Port . Lakini katika kuongea hayo mambo ya Lamu Port, kama vile Kenya Ports Authority (KPA) Mombasa, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}