GET /api/v0.1/hansard/entries/1129251/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1129251,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1129251/?format=api",
    "text_counter": 47,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "tunasema kwamba angeweka mkazo zaidi ya kwamba wale vijana wa Lamu ambao tangu tupate uhuru mpaka hivi sasa, kusema ukweli ni kwamba, wengi wa vijana wa Lamu hawajapata ajira. Nafasi ile ya Lamu Port, yeye kama Rais angeweza kutoa ishara ikiwa kama kuna kazi zozote kama za mikono ama za aina yoyote, zile ambazo si lazima watu waende skuli wapate, zingepewa vijana wa kutoka eneo lile la Lamu na pia kuona kwamba ikiwa zingine zitapatikana, basi zipewe Wakenya na hususan watu wanaotoka katika maeneo ya pwani. Vilevile biashara zinazotendeka katika maeneo yale ya kule Port, nafasi hizo zipewe wale watu ambao wanaishi katika sehemu hizo. Ni jambo la kusikitisha hivi leo tukiona ya kwamba kazi hizo zimepewa watu wengine ila si wale watu wa kutoka Lamu ama pwani. Bw. Spika, jambo la pili ni mabadiliko ya mazingira katika ulimwengu. Rais alienda kule na kushiriki katika mazungumzo ya Kongamano hilo na hayo pia aliweza kuyataja. Lakini kusema na kutenda ni vitu tofauti. Rais hakuweza kutenda. Hakuweka mipango na mikakati ya kisawasawa kuona kwamba maeneo yale ambayo yana janga la ukame---. Kuna maeneo mengi sana katika Kenya ambayo yamekumbwa na janga la ukame. Pengine kama mvua ikinyesha huwa inajaza maziwa na nyumba huharibika. Lakini nikiguzia upande wa pwani ni kwamba hatuna mafuriko yale ya ajabu lakini tuko na njaa. Mifugo hufa njaa ikikamilika. Na sio katika Kilifi pekee, bali katika maeneo ya semi-arid, ambayo huwa upande wa magharibi ama upande ule wa kaskazini nchini Kenya, huwa na janga kubwa sana. Katika maeneo hayo, mifugo wanakufa. Ukiangalia hususan ndani ya Kaunti ya Kilifi, kuna maeneo bunge matatu ambayo ni Ganze, Kaloleni na Magarini. Janga hili la njaa na ukame limeathiri watu na mifugo katika maeneo hayo matatu ya Bunge kwa kusababisha vifo kadhaa. Watu wameketi kama ambao si wa Kenya. Rais hakuweza kutamka na kusema ni njia gani ambayo Serikali itafanya kuona ya kwamba kila mwaka, ikiwa watu wanaweza kupoteza maisha, mifugo, biashara kuharibika na watu kufa kwa sababu ya janga la njaa, ni njia gani mbadala ambayo Rais ameiweka ambayo itaweza kusaidia sasa na hata siku za usoni kuona ya kwamba Kenya haikumbwi tena na janga la njaa. Hivi sasa, janga la njaa linaanza kuisha kwa sababu mvua imaeanza kunyesha, lakini je baada ya hii mvua kuisha, mwaka ujao tutakua na hili janga tena? Hilo ndilo swala kubwa. Bw. Spika, maoni yangu ni kwamba, Rais angekuwa na mikakati mbadala ya kusuluhisha tatizo la janga la njaa inayosababisha vifo vya mifugo na binadamu. Wakenya wana njaa ilhali Katiba inasema ya kwamba ni lazima watu wapate chakula ndani ya Kenya. Hapo Mhe. Rais hakufanya vyema. Vile vile ilikuwa inatakikana Rais afafanue matatizo yanayowakumba Wakenya katika sehemu totafauti tofauti. Katika maeneo ya pwani ama maeneo ya kaskazini mashariki, familia nyingi zina huzuni kwa sababu ya watu wanashikwa kiholela. Tumesema hapa mara kwa mara kwamba wanaoshikwa ni vijana wengi wa dini ya Kiislamu. Ijapokuwa watu wengine wanashikwa pia, waliozidi ni hawa wa dini ya Kiislamu. Hatuwezi kujua ni kwa sababu gani. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}