GET /api/v0.1/hansard/entries/1129252/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1129252,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1129252/?format=api",
"text_counter": 48,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Jambo la kusikitisha ni kwamba wakishikwa, hawapelekwi kotini, wanauawa kiholela. Baadaye tunapata familia zinalia na hatuelezwi ni sababu gani familia zimekosa watu ndani ya nyumba. Tukiangalia kwa kina, tunaona kwamba wengi wamepoteza maisha yao katika mikono ya polisi. Kila mara tunaambiwa waliouawa walikuwa wanaume au wavulana ambao walikuwa wanaenda kujiunga na kikundi haramu cha Al Shabaab. Bw. Spika, lazima tuzingatie sheria zetu za Kenya. Mtu amaposhikwa na polisi ni sharti apelekwe ndani ya korti. Rais wetu hakuweza kutamka mikakati ambayo ameweka kisawa sawa ya kwamba ataongea na Wizara ambayo inahuska, ili kutetea maisha ya hawa vijana ambao huwa wanapotea kutoka kwa manyumba. Tumechoka! Ikiwa watu wa Pwani watakua wakizika watu kila siku; mtu akipotea, mwili wake unapatikana baadaye katika kichaka fulani au mwili haupatikani kabisa, huleta majonzi katika familia nyingi. Ilikua muhimu Rais mwenyewe kutamka njia mbadala ambayo ameweka mbele ili kusitisha kupotea kwa maisha ya vijana hao wa Kiislamu. Ama hakutakua na watu kupotezwa bila kuonekana. Jambo hilo limeleta majonzi. Hutuwezi tukajua mtu amepotezwa au amepelekwa wapi. Tunazungumzia wapendwa waliozaliwa katika familia tofauti, wako na mama na baba zao, ndungu na marafiki zao ambao wanawapenda sana. Lakini utaona ya kwamba mtu akipotea katika familia hatuwezi kujua siku moja atakuja. Hatuwezi kujua kama tufanye ile kimila ya mtu aliyekufa au la. Hatuwezi kujua kama ameenda na hatutamuona tena. Inakua hofu na balaa katika familia. Kwa hivyo, Rais angeingilia kati na kuambia wale askari wawache tabia kama hizo ama wasifanye vitu kama hivyo kwa sababu ni kunyume na sharia za binaadamu. Bw. Spika, katika ujenzi wa barabara, Kaunti ya Kilifi ni vyema tumeweza kupata barabara. Tumepata barabara na namsifu Rais. Hapo alijiariibu kwa sababu tuko na barabara. Ukitoka Nairobi unaweza kupitia Salaget ukaingia Malindi. Unaweza kupitia Mariakani ukaingia Mavueni ukafika Kilifi. Ukitoka Mombasa unaweza kupita Kilifi ukapita mpaka Malindi, Magarini na ukaenda mpaka Lamu na kutakua na lami. Lakini wasifikirie tu kutengeza hizi barabara kwa upande wa utalii. Wafikirie kwamba kuna wenyeji wanaoishi katika maeneo ya pwani. Barabara zilizotengenezwa ni zile kubwa ambazo zinaweza kusaidia katika sekta ya utalii, haziwafai sana wenyeji wanaoishi katika maeneo yale. Wafanyibiashara na wakulima ambao wanakuza matunda yao na bidhaa zinginezo zinazohitajika kufika soko ya marikiti kwa haraka wanaumia. Bidhaa za wakulima hao vikifika soko ya Marikiti kwa haraka, wataweza kupata bei kwa sababu bado vitakua bado viko freshi. Kwa sasa, barabara zinatengenezwa kwa sababu tuna target ama nia yetu ni kusaidia watalii kufika Malindi na kuenda beach . Kwa sasa barabara hizo haziwasaidii wenyeji kufanya biashara zao na hio si sawa. Angeweka mikakati ya kisawa sawa kuona ya kwamba watu wote wanaoishi katika maeno ya pwani wamepata baarabara zao kisawa sawa. Bw. Spika, Mhe. Rais, katika Hotuba yake ya Kitaifa hakugusia janga la ufisadi; alilikwepa jambo hilo. Hapo naona Mhe. Rais alipata asilimia sufuri. Hakujaribu kabisa. Janga la ufisadi alilikwepa na hilo ndilo janga ambalo limefanya nchi hii kubaki nyuma.. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}