GET /api/v0.1/hansard/entries/1129253/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1129253,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1129253/?format=api",
"text_counter": 49,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Sijui ni kwa nini mpaka sasa wale walioiiba pesa za Covid-19 mpaka sasa hawajachukuliwa hatua. Hili Bunge lilileta ripoti yake. Ripoti ikapelekwa namna hii namna hii ikawa vile ilivyokua lakini kuna ushahidi wazi kabisa ya kwamba pesa za Covid-19 ziliibiwa. Walioiba wanajulikana wazi kabisa. Nampa kongole dadangu Senata Dullo na kamati yake maalum. Waliandika ripoti nzuri sana lakini ile ripoti yake mpaka hivi sasa hatua haijachukuliwa. Janga la ufisadi sio ya pesa za Covid-19 peke yake, katika kila sekta ya Serikali, kuna ufisadi. Hatua ambayo Rais angechukua hivi sasa ni kuweka mpango mbadala ili nchi hii iwe huru na ufisadi. Lakini Rais alikwepa jambo la ufisadi kwa sababu anazozijua yeye. Hivyo mimi nampa asilimia sufuri. Bw. Spika, la mwisho ni jambo la uchumi samawati. Uchumi samawati unaweza kusaidia maeneo ya pwani na yale ya Ziwa Victoria. Uchumi samawati ni muhimu sana. Na hata vile alivyosema ya kwamba hata inchi moja ya Kenya hataiwachilia ni kwamba sisi tutakua na bahari kubwa sana. Ziwa letu liko pale na linatoa samaki. Lakini faida ya ule uchumi samawati mpaka sasa bado haujapatikana; uko duni sana. Ijapokuwa mipango imefanywa ya kisawa sawa, bado bidii inatakikana iwekwe na mipango kisawasawa iwekwe ili iweze kufaidi mkenya. Lakini hivi sasa ukiangalia uchumi samawati au blueeconomy, ilioko pwani, haijasaidia mpwani kwa lolote. Saa zingine kule nyumbani tunasema pwani si Kenya. Na tuna sababu kwa nini tunasema hivyo. Ni kwa sababu mambo ambayo yanaweza kutengenezeka uchumi ndani ya pwani yamelegezwa kamba. Ni kwa sababu hizo watu wa pwani kila siku wanasema pwani si Kenya. Hivi sasa, mradi ulioanzishwa wa Standard Gauge Railway (SGR) ni shetani mkubwa maanake iliua uchumi wa Mombasa. Mombasa ni kiungo muhimu sana kwa watu wa pwani. Kutokea Lamu, Garissa, Isiolo na kila pahali. Bandari ya Mombasa inawafaa watu wote wa pwani. Lakini ukiangalia uchumi samawati na bandari zimekufa. Ukienda Momabsa sasa hivi, utashanga sana kwani Mombasa si kama vile ilivyokuwa zamani. Ilikuwa vibrant, na wenye uchumi unaendelea kisawa sawa lakini kwa sababu ya SGR tumefanyiwa matusi makubwa sana na hata mipango ile ambayo Rais alikua ameweka ya kisawa sawa haifanani na vile inaweza kusaidia uchumi samawati. Bw. Spika, la mwisho kabisa ni kwamba, yote haya tisa nimesema, la kumi ni kwamba, Hotuba ya Rais kidogo ilipeana moyo. Ilipeana moyo kwa Wakenya, kwamba, ijapokuwa yeye anaondoka katika miezi tisa ijayo, yale aliyoyafanya ni haya. Na---"
}