GET /api/v0.1/hansard/entries/1129415/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1129415,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1129415/?format=api",
    "text_counter": 18,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Pia mimi nataka niungane na wewe kwa kuwakaribisha wageni kutoka upande wa Narok, na kusema kwamba, wote waliokuja kujifundisha hapa na kujionea yanayoendelea hapa ndani ya Bunge la Seneti ni mambo ambayo ninauhakika wakati wowote wakirudi nyumbani wataweza kutafakari na kujua ya kwamba waliweza kupata faida ya kuja kutembelea Seneti. Ni jambo nzuri kuona watu kutoka Narok wamefika hapa leao. Wakati mwingi ni watu wa Nairobi ambao huja hapa. Watu wa kutoka kaunti kama ya Narok, Kilifi na kwingine, ni nadra kwao kupati nafasi kama hii ya kuja kutembelea Bunge la Seneti. Kwa vile ndugu yangu Olekina ambaye ni swahiba wangu mkubwa hayuko hapa, nachukua nafasi hii nikijua ya kwamba angekuwa hapa yapo mengi angeyasema. Hata hivyo, nitasema Narok is a great county . Ni kaunti moja katika Kenya ambayo iko na ushupavu. Ndani ya Bunge, inaongozwa na Sen. Olekina kama Seneta wa Narok. Kuna umuhimu kutambua kwamba utendakazi wake ndani ya hili Bunge la Seneti ni wa hali ya juu sana. Kila akisimama hapa yeye anatetea watu wa Narok. Ningependa kuunga mkono kwa usema ni wazo nzuri kwa wafanyakazi wa Bunge la Kaunti ya Narok kuja katika Bunge la Seneti ili kujionea mambo yanavyoendeshwa. Asante sana nikitumaini ya kwamba, watakapokuwa wakirudi nyumbani watakuwa wamejifundisha mengi kutoka kwa Bunge la Seneti."
}