GET /api/v0.1/hansard/entries/1129417/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1129417,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1129417/?format=api",
"text_counter": 20,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Malalah",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13195,
"legal_name": "Cleophas Wakhungu Malalah",
"slug": "cleophas-wakhungu-malalah-2"
},
"content": "mbunge wa Kaunti ya Kakamega. Nilikuwa naibu wa spika. Kuna changamoto nyingi sana ambazo wabunge wa kaunti hupitia. Sisi kama Maseneta tunafaa tuwasaidie ili waweze kufanya kazi yao vizuri. Mabunge za kaunti ni jukwaa nzuri ambayo inaweza kusaidia kukuza uongozi wa viongozi siku za usoni. Nimesema nilikuwa mbunge wa Bunge la Kaunti ya Kakamega na sasa hivi mimi ni Seneta. Hapa katika Seneti nimejifunza mambo mengi ya ugatuzi. Mwaka ujao nitawania kiti cha ugavana cha Kaunti ya Kakamega. Kwa hivyo, bunge za kaunti ni jukwaa inayokuza uongozi wa kila ngazi au kiwango chochote. Ninawahimiza MCAs wetu wajue jukwaa hii siyo ya mzaha na wanatakiwa kufanya kazi yao vizuri. Ni jukwaa linakupa mtu tajriba ya kutosha ya kuwania viti vingi hapa nchini baadaye. Mwisho kabisa, wakazi wa Narok, sisi tunakaa hapa na Mhe. Madzayo na Mhe. Olekina. Hamkufanya makosa kumchagua Seneta wenu kwa sababu yeye hutetea haki zenu na kushughulikia matakwa yenu kwa moyo wake wote. Jambo lolote ambalo linafanyika hapa kwenye Seneti na ambalo linahusu watu wa Narok na jamii ya Wamasai kwa kumla, yeye hakosi kuchangia. Endeleeni kumshika mkono kwa sababu yeye ni kiongozi ambaye atasaidia nchi hii siku za usoni Bi. Spika wa Muda, kwa hayo machache, ninawakaribisha wageni wetu katika Seneti. Mwenyezi Mungu awabariki sana."
}