GET /api/v0.1/hansard/entries/1129439/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1129439,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1129439/?format=api",
    "text_counter": 42,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Ni jambo la kusikitisha sana katika hii Petition ambayo imeletwa hapa katika hili Bunge la Seneti. Nawapa kongole wale waliokuwa na imani na nguvu ya kuona ya kwamba ni lazima jambo hili lifike katika Bunge la Seneti. Seneti itaangalia yale maovu yanayotendwa na Gavana akijifikiria ya kwamba hakuna sheria. Anafikiri yeye ndiye sheria ya mwisho. Kuna sheria na watu wa huko Nyandarua wako na imani nayo. Ni jambo la kusikitisha kuona ya kwamba mtu anaweza kusimamisha kaunti nzima kutoendelea kwa sababu. Ukisimamisha County Assembly ni kama umesimamisha kaunti ya Nyandarua na hakuna kazi yoyote itakayo endelea bila idhini yake. Hauwezi, hata kidogo, kusimamisha matendo ama vile Bunge itakavyofanya kazi yake. Ni jambo la aibu au kusikitisha kuona ya kwamba watu ambao ni majangili, wasiofanya kazi pale au kuhusika pia wamepewa nafasi ya kwenda ndani ya maofisi, kuangalia, kutembea na kufanya vile wanavyotaka. Hakuna sheria inayokubalia gari ya Spika kutumiwa na wananchi ambao hawafanyi kazi ndani ya bunge ya kaunti ama bila idhini yake. Haiwezi kutumika kwa sababu gavana amesema itumike na mtu fulani. Kuna mengi ambayo yameweza kutanguliwa katika hiyo Petition. Tunaona kunao umuhimu wa Bunge la Seneti kuingilia kati na kuchukua hatua kuona ya kwamba hilo Bunge la huko nyumbani limeweza kurudi katika hali yake ya kawaida na kuendelea kusaidia wananchi. Asante, Bi Spika wa Muda."
}