GET /api/v0.1/hansard/entries/1129572/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1129572,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1129572/?format=api",
    "text_counter": 175,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Asante sana. Nashukuru sana kwa sababu nakuona Spika, umechukua hatamu zile nilikuwa nazo kwa hivyo kongole sana kwa sababu lazima tuendeleze Kiswahili kwa sababu ni lugha ya Kitaifa ambayo ni nzuri zaidi. Nashukuru kurudi hapa tarehe moja Decemba kwa sababu naona kwamba ni jambo la muhimu, hata ingawa naona taa ya manjano imeweza kuwekwa lakini niseme kama singekuwa na mawakili gushi, singewahi rudi hapa. Kwa hiyo, taarifa hii ambayo imewasilishwa na Mweshimiwa Senata wa Nandi, Cherargei, ambaye pia ni wakili, ni muhimu sana kuhakikisha ya kwamba hatuna matapeli ambao wanajifanya kama wao ni mawakili alafu kazi yao ni kuchukua hela za watu na hawaendi kotini. Kwa hivyo ni jambo ambalo linafaa kushughulikiwa zaidi. Nafikiri kumekuwa na tashwishi sana katika lile shirika la mawakili la Las Society"
}