GET /api/v0.1/hansard/entries/1129574/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1129574,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1129574/?format=api",
    "text_counter": 177,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Nilikuwa na Rais, Bwana Havi. Nina waomba wachukulie hili jambo kuwa muhimu sana kwa sababu tunajua kama mtu yeyote angependa kupata haki, lazima awe na wakili mzuri ili akwende katika kitengo cha mahakama na aweze kuskizwa. Lakini kama mtu yeyote ambaye anafanya biashara zingine zozote anaweza pia kujisimamisha kama wakili na kufanya shughuli ambazo sio za rasmi kwa sababu ni kampuni tu, itakuwa ni jambo ambalo ni la kudhoofisha usawa wa sheria. Bw. Spika wa Muda, ningependa pia kuchukua mwito huu kusema kwamba, ni vizuri pia mawakili nao wasiwe wanatumia kampuni zao za uwakili kufanya biashara zingine. Nafkiri hiyo ndiyo taswishi ambayo ipo kwa sababu kampuni ya mtu binafsi ina nafasi ya kufanya chochote kile ilhali pia biashara ya uwakili inafaa kusajiliwa rasmi. Naunga mkono."
}