GET /api/v0.1/hansard/entries/1129907/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1129907,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1129907/?format=api",
"text_counter": 136,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Hali ya taasisi za kiafya katika kaunti zetu imeimarika kwa sababu ya kujitayarisha na janga hili la korona na bado janga hili halijakwenda. Inafaa tuwe macho ili kuhakikisha janga hili lisiturudie tena. Katika Hotuba yake, Mhe. Rais ameangazia mambo mengi ambayo yanaonyesha kwamba baada ya kushirikiana na Mhe. Raila Odinga, Waziri Mkuu wa Zamani, imeonekana hali ya nchi imekuwa tulivu, usalama ukaimarika na watu wanaendesha mambo yao na kushukisha joto la kisiasa ambalo tunaona limeanza kupanda tena."
}