GET /api/v0.1/hansard/entries/1129924/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1129924,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1129924/?format=api",
"text_counter": 153,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, kwa kumalizia pia ni kwamba, tumeona kuwa maswala ya usafirishaji wa mizigo ni njia moja ambayo itasaidia Wakenya kuweza kujikomboa, hususan watu wa Mombasa na wengine ili kuweza kupata biashara katika kaunti zetu. Ukiangalia mkondo wa barabara kutoka Mombasa mpaka Malaba, kuna biashara nyingi ambazo zinafanyika katika barabara hiyo. Biashara zile ninawezakufilisika iwapo hatutaweza kuwa na usafirishaji wa mizigo kwa njia nyingine mbali na njia ya reli. Nikimalizia, bado tuna changamoto nyingi ambazo nchi inatakikana kuzikabili na kuziepuka. Changamoto hizi tunaweza kuzikabili tu wakati nchi yetu itakuwa na amani. Tutakuwa tunavuta Kamba katika sehemu moja. Hususan huu wakati ambao tunakwenda katika maswala ya kura, inafaa tuangalia kwamba ijapo kuwa tunapigania viti, lengo letu ni kwamba Kenya iweze kubakia nchi moja. Asante Bi Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii."
}