GET /api/v0.1/hansard/entries/1129926/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1129926,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1129926/?format=api",
    "text_counter": 155,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante sana Bi. Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii niweze kuunga mkono Hotuba ya Rais aliyoisoma jana Bungeni. Kusema kweli Hotuba yenyewe ilikuwa nzuri sana. Mimi kama Seneta wa Kaunti ya Kwale kwa niaba pia ya watu wa Kwale natoa shukrani zetu kubwa sana. Ukiangalia upande wa barabara, haswa katika Kaunti yetu ya Kwale, kuna barabara zingine ambazo kutoka wakati wa ukoloni zilikuwa hazijawahi kupata lami. Nitataja hapa kwamba kuna barabara kuanzia Kanana mpaka Shimoni ambayo kwa miaka yote kutoka tupate uhuru ilikuwa haijatiwa lami. Lakini kwa kupitia kwa Rais na Serikali yake, hii barabara imeweza kutiwa lami. Hivi sasa kutoka Kanana mpaka Shimoni ni lami moja kwa moja. Bi. Spika wa Muda, barabara nyingine katika Kwale ambayo sisi wakaazi tunamshukuru Rais na Serikali ni kutoka Majoreni mpaka Vanga. Barabara hii imekaa kwa miaka mingi sana bila kuwa na lami. Kwa hivyo, tunatoa shukrani kubwa sana kwa Rais na Serikali yake kuweza kututilia hiyo lami. Barabara nyingine ni kutoka Lunga Lunga mpaka Vanga. Hii ni barabara ambayo imekuwa bila lami kutoka wakati wa uhuru, toka mimi sijazaliwa lakini. Kupitia Serikali hii ya Rais barabara hizo zimetiwa lami. Kuna barabara ya Samburu mpaka Kinango. Saa hii ukitoka Nairobi na unataka kwenda Kwale ama Diani, huna haja ya kwenda moja kwa moja mpaka Likoni. Unapitia Samburu na kwenda moja kwa moja mpaka Kinango. Barabara kutoka Kinango mpaka Kwale inatiwa lami saa hii. Kwa hivyo, Hotuba ya Rais aliyozungumzia ni Hotuba ambayo mimi mwenyewe kama Seneta wa Kwale ambaye pia ni Mbunge katika Seneti, ilikuwa ni nzuri sana. Bi. Spika wa Muda, ukiangalia upande wa umeme, kuna sehemu zingine katika Kaunti ya Kwale ambako watu walikuwa hawajawahi kuona umeme kutoka wakati wa uhuru. Leo ukiwasha kidude, umeme unaonekana. Sehemu za Muhaka, Kilole na Msambweni huko ndani, kuna umeme. Tukizingatia mambo ya elimu, Alhamdulillahi kusema kweli imeboreshwa na shule kutengenezwa. Hivi juzi Rais alisema kwamba shule za upili zingine ziweze kujengwa tena. Kwa hivyo, Hotuba yake imegusia kila kitu katika nchi hii. Ni Hotuba ambayo ni safi kabisa na kila Mkenya anaiunga mkono. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}