GET /api/v0.1/hansard/entries/1129927/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1129927,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1129927/?format=api",
"text_counter": 156,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, ni kawaida kwa binadamu wengine kutoridhika na kila jambo siku hizi. Utasikia mwingine anasema hivi na vile, lakini kongole kwa Rais. Mwenyezi Mungu amjalie aweze kutengeneza zile ambazo ametarajia kutengenezwa na ziweze kuendelea na kumaliza hizo shughuli. Mungu akipenda kila kitu kitakuwa sawa sawa. Sitaki kusema mengi kwa sababu mengi yamezungumzwa hapa. Yangu ni kutoa shukrani kwa ile Hotuba yake aliyosoma Bungeni jana na mengi ambayo yamezungumzwa hapo. Ukiangalia mambo ya afya, saa hii akina mama ambao wengine hawana uwezo wanakwenda kujifungua hospitalini. Ukifika hospitali za kwetu huko sehemu za Msambweni, Lunga Lunga, Silaloni na Kinango huko, akina mama wanaenda kujifungua wengi sana bila shida. Kwa hivyo, tunampa kongole kubwa sana Rais. Hotuba yake ilkuwa safi kabisa na tunamshukuru. Kuna wengine ambao wanazungumza tu kwamba ilikuwa hivi na vile, lakini mimi naona kuwa mambo yako sawa kabisa, ukiangalia mambo ya maji, barabara, elimu na afya. Asante sana kwa kunipa fursa hii."
}