GET /api/v0.1/hansard/entries/1132669/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1132669,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1132669/?format=api",
    "text_counter": 127,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Spika. Ningependa kuchukua fursa hii kuungana na wenzangu kumshukuru Mhe. Rais na kumpongeza pakubwa kwa Hotuba yake hapo jana katika Bunge hili. Ni dhahiri shahiri kuwa mengi yaliyozungumzwa na Mhe. Rais ni mambo ambayo yameonekana na Wakenya. Jambo moja kubwa ambalo lilishuhudiwa na Wakenya katika Bunge lililopita nikikumbuka vyema ni kuwa katika shughuli kama hii ya Hotuba ya Rais, Bunge lilikuwa na taharuki kubwa na bughudha nyingi sana kutokana na hali za kisiasa. Ukweli ni kwamba, jana kulishuhudiwa utulivu uliotokana na ushirikiano mwema kati ya Mhe. Rais Uhuru Kenyatta na wapinzani wake. Hata hivyo, ningependa kumwambia Mhe. Rais kwamba katika kutembea na hawa viongozi, afahamu kuwa mambo ya siasa ni kuwa unapojaribu kutengeza hili, usiharibu lingine. Naamini pakubwa kuwa haya yamepatikana kupitia ushirikiano wake mwema na Naibu wake, Mhe. William Ruto. Imedhihirika wazi kuwa maswala ya miundo msingi pamoja na barabara zinazojengwa Nairobi na Mombasa katika maeneo ya Kipevu na Changamwe kuelekea airport ni juhudi za Mhe. Rais, akisaidiana na Naibu wa Rais, katika Serikali hii inayoongozwa na hao wawili. Hali halisi kuhusu mengi ambayo yamezungumziwa na Mhe. Rais imeonekana na Wakenya, lakini bado tuko na changamoto za hapa na pale. Nikizungumzia eneo Bunge langu la Lamu Mashariki katika Kaunti ya Lamu, tunashukuru Mhe. Rais kwa juhudi zake. Kuna barabara ambazo zimetengenezwa kutoka Garsen hadi Mokowe. Rais ametilia mkazo maswala ya Lamu Port-South Sudan-Ethiopia-Transport Corridor (LAPSSET). Kuna umuhimu mkubwa katika hali hizi kuzingatiwa na kuwa karibu na washauri watakaotoa ushauri mwafaka wa kumaliza hilo jambo ambalo wamelifanya kwa njia nzuri. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}