GET /api/v0.1/hansard/entries/1132670/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1132670,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1132670/?format=api",
    "text_counter": 128,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Ningependa kumwambia Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta kuwa, mbali na kuona miradi mingi ya barabara ikifanyika, katika Eneo Bunge la Lamu Mashariki, hakuna hata kilomita moja ya lami. Nimeweza kulileta jambo hili mara kadhaa katika Bunge hili na kuliwasilisha kwa wahusika wakuu. Kama viongozi kutoka Lamu, tumeshuhudia ujenzi wa LAPSSET. Ni matarajio makubwa kuwa kutokana na malengo ya ujenzi wa poti ile, Serikali hii na Rais watawapea kipao mbele vijana wetu wa Lamu katika nafasi zitakazopatikana mahali pale. Hayo ndiyo mambo ambayo yanafaa kuwa na mwongozo mwema katika Serikali hii tunayo. Tatizo kubwa ambalo liko na yafaa tulizingatie ni kuwa katika yote haya yanayofanyika, pesa zinazotumika katika miradi mingi ni pesa za madeni ya mikopo inayochukuliwa kutoka kwa mataifa ya nje. Kuna umuhimu wa Serikali kuhakikisha ya kwamba tumedhibiti madeni haya kwa sababu ya siku zijazo. Vile vile, kutokana na haya, ni muhimu Serikali iwe na mikakati mwafaka ya kupambana nayo. Kwa mfano, Mhe. Rais alilizungumzia swala la ukame. Twajua kwamba kuna ukame katika sehemu nyingi nchini na…"
}