GET /api/v0.1/hansard/entries/1132685/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1132685,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1132685/?format=api",
"text_counter": 143,
"type": "speech",
"speaker_name": "Rabai, ODM",
"speaker_title": "Hon. William Mwamkale",
"speaker": {
"id": 2672,
"legal_name": "William Kamoti Mwamkale",
"slug": "william-kamoti-mwamkale"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Spika kwa nafasi hii. Nasimama kujiunga na wenzangu kumpongeza Rais kwa Hotuba hii ambayo ni matakwa ya Sheria Kifungu 10 cha Katiba yetu. Rais ametekeleza yale ambayo ameweza kuyatekeleza na ni lazima yapelekwe kwa wananchi ama watu waambiwe kile ambacho kimefanyika. Kwanza, Mhe. Spika, nataka nimpongeze Rais kwa yale aliyofanya kwa upande wa miundo msingi ndani ya nchi hii. Miundo msingi ni infrastructure . Rais amejaribu ingawaje kuna mengine ambayo akiyafanya, atatekeleza ama atawacha wosia ulio kamili. Kwa bandari, Rais amejaribu. Bandari ya Mombasa ameipanua vizuri na imebadilika sura. Ametupatia pia bandari mpya Lamu. Kitu ambacho tunamuomba Rais akamilishe wosia wake ni kuhakikisha kwamba bandari hizi zinanufaisha wakaazi ambao wanazunguka bandari hizi. Kama watu wa Pwani, hicho ndicho kilio chetu. Ijapokuwa bandari imebadilika, kuna kazi ambazo zimehamishwa na masuala kama clearing and forwarding sasa zimeenda Naivasha. Tunamuomba Rais akamilishe wosia wake kwa kuhakikisha kwamba kazi ambazo zilikuwa zikifanywa ndani ya Bandari ya Mombasa, zinaendelea kufanywa na kutekelezwa pale. Vile vile, katika miundo msingi, tunashukuru kwamba ameleta Standard Gauge Railway (SGR) na tunaomba hiyo nayo ipewe maagizo. Isiwe tu ni lazima mizigo yote ifikishwe Naivasha hata kabla ya kushughulikiwa. Tunaomba ahakikishe kwamba mizigo inayobebwa ni yale ambayo haihitajiki ama wenyewe hawatoki Mombasa. Kwa wale ambao wanatoka Mombasa, mizigo ile ishukishwe Bandari la Mombasa. Huko ndio kujivunia. Wakenya watajivunia ya kwamba wana muundo msingi huu ambao unatunufaisha. Kwa upande wa mabarabara, tunamshukuru Mheshimiwa Rais. Ukienda Mombasa saa hii, ukifika Kibarani, kazi inaendelea. Tuna imani kwamba hii ikimalizaka, Mombasa itakuwa imebadilika. Hata tukimpongeza Rais Kibaki, ukweli wa mambo ni kuwa ukija kwa mambo ya miundo msingi, hakuna kwa sasa hivi ambaye ametekeleza na kubadilisha kama Rais Uhuru."
}