GET /api/v0.1/hansard/entries/1132688/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1132688,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1132688/?format=api",
"text_counter": 146,
"type": "speech",
"speaker_name": "Rabai, ODM",
"speaker_title": "Hon. William Mwamkale",
"speaker": {
"id": 2672,
"legal_name": "William Kamoti Mwamkale",
"slug": "william-kamoti-mwamkale"
},
"content": "Linda Mama ni jambo ambalo limegusa watu wengi. Sisi kama Wabunge huwa tunafuatwa na kila mtu wakati wanapokuwa wagonjwa. Hata mama akienda kujifungua anatufuata. Lakini Linda Mama imetupumzisha sisi Wabunge. Imepumzisha viongozi na inafanya kazi nzuri. Kwa hivyo, tunapongeza na tunasema: Mgalla muue na haki yake umpe. Jamani, hakuna aliye kamili. Aliyoyafanya Rais Kenyatta, yamegusa Wakenya. Tupende tusipende si lugha nzuri, lakini Mgalla muue, na haki yake umpe. Ahsante sana, Mhe. Spika."
}