GET /api/v0.1/hansard/entries/1132712/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1132712,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1132712/?format=api",
    "text_counter": 170,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Samburu CWR, KANU",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Maison Leshoomo",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi ili niungane na wenzangu kumshukuru Rais wetu, Uhuru Muigai Kenyatta, kwa kazi ambayo amefanya. Mhe. Spika, kusema ukweli, Rais alitaja sekta zote katika nchi hii ambazo amefanyia kazi. Kila Mkenya ameona kile Mhe. Rais amefanya. Katika utawala wake, amefanya mengi. Ni vyema tujue kama Wakenya kuwa wakati alichukua usukani kama Rais, alipata wakati mgumu sana. Hii ni kwa sababu alichukua usukani akiwa bado na kesi kule Hague na pia hali ya usalama ilikuwa imedorora. Kwa hivyo, ameweza kufanya kazi miaka minne tu pekee. Katika miaka minne, kila Mkenya ameona kile Rais amefanya. Sisi kama Kaunti ya Samburu, kwa miaka hamsini, tulikuwa tukianza safari na kusema tunaenda Kenya. Hatukuwahi ona chochote ambacho wenzetu walikuwa wameona. Tumeona maendeleo haya wakati wa Rais Uhuru Muigai Kenyatta. Tumeona stima, lami na hati miliki za mashamba ambazo hatujaziona kwa miaka hamsini. Kenya imeona tofauti kubwa tangu Rais Uhuru achukue usukani. Rais alitaja idara ya usalama. Afisa wetu wanaweza kupata huduma za hospitali kila mahali. Sisi ndio tunawaona afisa wa serikali wakiumia wakati wa vita. Wanapopata ajali na kuumia, hakuna hospitali iliyo karibu ambayo wanaweza kupelekwa. Mambo hayo yote yametugusa mioyo. Rais anapostaafu, bado atakuwa na nafasi ya kuiangalia Kenya na macho mawili. Bado yeye ni mchanga na atakuwa akituangalia na ikiwa Kenya itaelekea pabaya, atairudisha pamoja. Jambo lingine ni lile la “ Handshake”. Nilikuwa kati ya wale waliotembea kaunti 47 tukitafuta umoja wa Kenya kama alivyotutuma Rais. Wakenya walitoa maoni ambayo wangependa kuwekwa katika sheria ili iwalinde. Inafaa kueleweka kuwa Rais hakuwa anatafuta mwanya wa kurudi katika Serikali au kubadilisha Katiba. Wakenya ndio walitaka mabadiliko yanayowahusu. Bado tunahitaji Building Bridges Initiative (BBI) irudi kwa sababu ni ya Wakenya; sio ya mtu binafsi. Wakenya ndio waliotoa maoni yao. Pia, tunashukuru Mhe. Raila Amollo Odinga kwa sababu hatungefika hapa sasa hivi isingekuwa “Handshake”. Kila mtu anajua hilo na usipo sema ahsante, Mungu atampa mtu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}