GET /api/v0.1/hansard/entries/1132803/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1132803,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1132803/?format=api",
    "text_counter": 261,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ruiru, JP",
    "speaker_title": "Hon. Simon King’ara",
    "speaker": {
        "id": 13468,
        "legal_name": "Simon Nganga Kingara",
        "slug": "simon-nganga-kingara-2"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia mwanya huu kuchangia kuhusu hali ya taifa iliyoletwa mbele yetu na kiongozi wa nchi hii jana. Kwanza kabisa ni kumshukuru kwa sababu ya kuheshimu Bunge na sheria. Aliona ni vizuri atumie utaratibu uliotengwa kikatiba kutekeleza kazi aliyopewa na wananchi. Kama vile wenzangu wamechangia hapo mwanzo, ni vizuri kuheshimu kwa kuongea yale mema na mazuri yametendwa na viongozi, hasa Uhuru Kenyatta. La muhimu sana, ndio tuweze kutekeleza maendeleo ya aina yoyote, ni vizuri tuwe na barabara za kupitia. Mnajua amechukua changamoto kubwa kuona kuwa barabara zimetengenezwa kwa wingi. Vilevile, kazi haiishi kwa siku ya kwanza. Barabara nyingi zimetengenezwa ingawa kuna zile mbili au tatu ambazo zimebaki. Hiyo si kusema kuwa kazi haijafanywa. Ukiangalia kwangu Ruiru, barabara zimejengwa lakini kwa sababu ya wingi wa watu, bado kuna barabara kama ile ya Rainbow kwenda Gikumari na kushikanisha Juja na Ruiru; ambayo bado tunatarajia itengenezwe katika utaratibu ule. Vilevile, mwanadamu hawezi kuishi bila maji. Serikali imechukua jukumu la kuhakikisha wananchi wengi hapa Kenya wamepata maji. Mimi siwezi lalamika. Hata kama maji hayajafika kwangu kote, najua kuna bwawa Ruiru litakalosaidia watu wa Ruiru, Juja, Thika na mji wa Nairobi. Ni vizuri kutambua hayo. Kwa afya, nimesimama hapa mbeleni na kuchangia hayo mambo. Tulikuwa na changamoto kubwa sana pale Ruiru kuhusu vitanda hospitalini. Tuko watu 600,000 na vitanda vilikuwa 24. Saa hii nimesimama mbele ya Bunge kusema ya kwamba kutokana na maendeleo mema ya Uhuru Kenyatta, tuko na vitanda 150. Hilo ni jambo nzuri. Na hatuwezi kusita kusema ukweli juu ya yale yametendeka. Ni vizuri vilevile kuhakikisha kuna amani ndio watu wafanye kazi pembe zote za Kenya. Kiongozi wa nchi amejaribu pale angeweza kuleta uwiano. Ndio sababu tuko hapa na unaweza fanya biashara katika pembe yoyote ya Kenya na maendeleo yanoge. Hata wakati kiongozi wa nchi na viongozi wengine walikuwa wanajaribu kuleta maendeleo Kenya yetu, tulikumbwa na hili janga la Korona. Mwendo wa maendeleo ulipungua. Lakini Serikali, ikiongozwa na Uhuru Kenyatta, ilipambana kuhakikisha angalau watu hawataangamia wote. Alisukuma na tukapata chanjo za bure. Hilo ni jambo hatuwezi kusahau kwa sababu afya inafaa kuangaziwa vizuri. Uhaba wa kazi ni changamoto. Serikali imejaribu kuhakikisha vijana wamepata kazi. Lakini lile liliniguza ni taasisi ya kiufundi, ukipenda TTI, ambayo imewekwa karibu maeneo yote. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}