GET /api/v0.1/hansard/entries/1132820/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1132820,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1132820/?format=api",
"text_counter": 278,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": " Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Ninasimama pia hapa niweze kuzungumzia Hotuba ya Mheshimiwa Rais ambayo aliweza kuzungumzia kuhusiana na taifa letu la Kenya. Na niweze kusema haswa nimenukuu sehemu ambazo tumeona amestawisha sana katika taifa letu la Kenya haswa katika mambo ya miundo misingi; mambo ya barabara. Na niweze kusema, mimi nikiwa natoka pale eneo la Likoni, tumeweza kupata barabara ya Dongo Kundu, ile tumeita Dongo Kundu Bypass . Na nafikiri kufikia Januari, Mheshimiwa Rais ataweza kuja kufungua ile barabara. Na ninajua ile barabara itaweza kutusaidia sana katika uchukuzi na kuweza pia kupunguza msongamano katika kile kivuko cha pale Likoni. Mheshimiwa Rais pia ameweza kutengeneza barabara nyingi sana katika taifa letu la Kenya haswa katika kipindi hiki chake cha pili. Tunaona barabara nyingi sana kule Thika na sehemu nyingi za Kenya. Hata ukiwa pale Mombasa ukiwa unatoka katika sehemu ya Airport The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}