GET /api/v0.1/hansard/entries/1132821/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1132821,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1132821/?format=api",
    "text_counter": 279,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "utaona miundo msingi wa barabara umeweza kuimarishwa sana. Vile vile hapa kwetu Nairobi kutoka Airport, katika ile Mombasa Road tunaona kuna ukarabati mkubwa wa hali ya juu sana katika mpango wa barabara. Vile vile pia tuliweza kupata ile bridge ambayo inaolea. Ambayo inaweza pia kutusaidia katika msongamano na haswa wakati janga la Korona lilivyokuwa limechacha sana, tuliweza kujengewa mvuko ule kwa muda mfupi sana. Kwa hivyo, ni asante sana kwa Mheshimiwa Rais. Vile vile pia katika mpango wa uchumi wa samawati, tumeona kwamba pale sehemu ya Liwatoni kuna ile tunaita kwa Kiingereza Fish Park, mahali ambapo kutakuwa kunafanyika biashara nyingi sana na shughuli nyingi sana za mambo ya samaki. Isitoshe, tunajua kama Wapwani na watu wa kule kwenye maji, sana tunategemea uchumi huu wa samaki. Kwa hivyo, jambo hili litaweza kuboresha wavuvi wetu na kina mama wetu pia wanaofanya biashara za samaki. Vile vile pia tunaona ya kwamba tuliweza kupata reli. Japo kuwa tunaona hii reli inatusaidia katika uchukuzi, lakini tuna changamoto kiasi tukiangalia bandari yetu na pia tukiangalia kampuni ya Railway ambayo pengine waliweza kuwa katika hii mikataba ya mambo hii ya Standard Gauge Railway ( SGR) ama mambo ya kupita na reli ama usafiri wa reli. Kwa hivyo, ningeomba tu Mheshimwia Rais pamoja na Serikali waangalie mbinu na njia ambazo tutaweza kusaidia taasisi hizi mbili, taasisi ya bandari ile ambayo ni Kenya Ports Authority (KPA) na taasisi ya reli ile ambayo ni Kenya Railway . Hii ni ili wasiweze kupata shida katika kulipa loni hii ambayo tuliweza kuichukua katika ile banki kule Uchina, inayoitwa Exim Bank ili tuweze kuendelea na uchukuzi wetu na pia taasisi zetu ziweze kufanya kazi zao ili Wakenya wetu wasipoteze ajira zao. Vile vile pia, hivi sasa kuna mpango wa kutengeneza kiwanda cha samaki katika sehemu za pwani na tunajua kiwanda hiki kitaweza kujenga ajira na pia kuboresha uchumi katika taifa letu la Kenya. Vile vile katika hiyo samawati tuna ile Port ya Lamu na tunajua sisi wote pale pwani na Kenya kwa jumla tukiwa na hii Port, itatuboreshea biashara katika sehemu za nchi jirani na hata sehemu za ng’ambo zile za nchi zingine za nje. Ili tuweze pia kuboresha uchumi na pia kujenga ajira na pia kujenga maendeleo katika sehemu zetu. Jambo la afya haswa nikiangalia Linda Mama, program hii, inafanyika kikweli na kina mama hawalipi chochote na wanaweza kuzaa bila malipo. Mambo yale ya kuleta umeme katika sehemu zile za mashambani pia yamefanyika na yamekuwa bora zaidi. Kwa mambo ya elimu, watoto kusoma na kuweza kupata asilimia 100 kwa watoto wanaotoka katika shule za primari na shule za msingi na kwenda katika shule ya msingi ni jambo bora. Jambo hili pia tunaona limefanyika. Vitabu pia watoto wamepata na pia tuna programu ambayo inamuwezesha mtoto aweze kupata ujuzi, aweze kuwa na uvumbufu na aweze kujua mambo zaidi na kuweza kujitegemea haswa pia wakati amemaliza shule. Najua janga la Korona lilikuwa changamoto lakini tunaona Mheshimiwa Rais alijaribu sana kuhakikisha vifo vitakuwa vichache..."
}