GET /api/v0.1/hansard/entries/1133871/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1133871,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1133871/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "North Imenti, JP",
    "speaker_title": "Hon. Rahim Dawood",
    "speaker": {
        "id": 2572,
        "legal_name": "Abdul Rahim Dawood",
        "slug": "abdul-rahim-dawood"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Naibu Spika. Kwanza, Ningependa kumpongeza Rais Wetu, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kwa yale aliyotuletea jana. Nikimuunga Rais mkono, nashukuru wenzangu ambao wamezungumza wakimuunga Rais na nimeshangaa leo Mhe. Sankok amemsifu Rais. Hicho ni kitu ambacho singeamini kabisa kama singemwona hapa. Kama ni sauti, ningefikiria ni ya mtu mwingine. Lakini, vile Rais alizungumza jana, nashindwa mtu aliye na macho haoni na aliye na masikio, hasikii. Kwa miaka minane, kazi ambazo amezifanya zimepita zile ambazo zilifanywa kwa zaidi ya miaka mia moja. Kama ni barabara, miaka mia moja tulikuwa na barabara kilomita elfu kumi na moja. Katika Uongozi wa Rais Kenyatta kwa miaka minane, tumekuwa na zaidi ya kilomita elfu kumi. Umeme umeunganishwa kwingi kuliko miaka hizo zote. Sisemi kuwa hatuhitaji umeme au barabara. Bado tunahitaji. Wakati Rais alichukua uongozi mwaka wa 2013, alisema kuwa iwapo hawatarudia kura tena, bilioni sita ambayo ingetumika kwa kura itawekwa kwa Uwezo Fund. Mhe. Naibu Spika, baadhi ya Wajumbe waliokuwa kwenye Bunge lililopita waliwaambia watu wao kwamba pesa hizo ni za bure na wasilipe. Lakini kuna wengine ambao wako hapa na wengine wapya waliokuja na kupata pesa ziko nyingi. Kwa mfano, katika eneo Bunge letu, tulipatiwa milioni kumi na sita lakini tumepeana zaidi ya milioni arobaini. Ikiwa Rais Kenyatta hangependekeza maneno hayo, hatungekuwa na pesa hizo za Uwezo Fund . The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}