GET /api/v0.1/hansard/entries/1133872/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1133872,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1133872/?format=api",
"text_counter": 107,
"type": "speech",
"speaker_name": "North Imenti, JP",
"speaker_title": "Hon. Rahim Dawood",
"speaker": {
"id": 2572,
"legal_name": "Abdul Rahim Dawood",
"slug": "abdul-rahim-dawood"
},
"content": "Vile vile, katika Uongozi wa Uhuru Kenyatta, National Health Insurance Fund (NHIF) imeweza kulipia wagonjwa zaidi ya laki tano ama zaidi ya watu wakiwa wanafanyiwa oparesheni na hata wakati wa kwenda ng'ambo. Kama sio Rais Uhuru Kenyatta, ni nani? Nimeskia mwenzangu akilalamika kwamba tumeongeza deni. Ni ukweli kuwa deni limeongezwa. Lakini ukimuuliza deni limeongezwa limeenda wapi? Atakuambia hajui ilhali anataka maji, umeme, barabara na kila kitu. Kwani hizo zitatoka bila pesa? Lazima pesa zikopwe ndipo vitu vitengenezwe? Wengine wamesema kuwa mambo ya ufisadi hayakuzungumziwa. Lakini wale ambao wanafaa kuangalia mambo ya ufisadi wanataka kumfunga Director of CriminalInvestigation (DCI) wetu, Bwana Kinoti kwa sababu ya kushika bunduki. Hana ile bunduki na wanataka ashikwe afungiwe Kamiti. Afungiwe kwa nini? Yeye ndiye anafanya ile kazi ya kushika. Hawa ni wale wafisadi wanaotaka afungwe. Mhe. Naibu Spika, nimeskia mambo ya Independent Electoral and Boundaries"
}