GET /api/v0.1/hansard/entries/1133898/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1133898,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1133898/?format=api",
    "text_counter": 133,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": "Pili, kiwango cha walimu walioajiriwa katika muhula wake ni kikubwa mno. Sisi pia tunataka kumwunga mkono na kumshukuru kwa sababu watoto wetu waliohitumu kama walimu nchini, wamepewa nafasi zao. Namshukuru Rais pia kwa kazi yake katika sekta ya ukulima. Alizingatia mambo ya wakulima wa chai waliokuwa wanapata pesa duni. Sasa hivi, wakulima wa chai wanapata haki yao. Aidha, Rais alisahau kuwa pia kuna wakulima wa mahindi kutoka sehemu kama Trans Nzoia. Ni kweli kuwa mbolea ilisambazwa kwa bei nzuri lakini wakulima kutoka sehemu ya Trans Nzoia wanahitaji usawa na wakulima wengine. Kwa mfano, Mhe. Rais alisema kuwa wakulima wa miwa wamepewa fedha. Wanastahili kuongezewa fedha zingine kwa sababu wakulima kutoka upande wa magharibi wameumia mno na hata watoto wao hawaendi shule kwa sababu ya mambo ya sukari. Nilipendezwa pia na mambo ya maternity . Nashukuru kwa sababu akina mama ambao hupata matatizo wanapolazwa katika hospitali zetu wakati wa kujifungua, wameongezewa pesa kutoka Ksh2,500 hadi Ksh30,000. Hilo lilinifurahisha kwa sababu akina mama, hata wale wanaotoka katika eneo langu, wamekuwa wakijifungua katika mazingira yasiyo bora. Pia, watoto wetu wanaopata mimba wakiwa wangali wachanga walikuwa wanapata shida sana wakati wa kujifungua. Sasa hivi, nafurahia kwa sababu watapata nafuu. Nikirejelea pesa za wazee, nitokako, kuna wazee ambao walikuwa hawapati pesa za uzeeni. Sio wote walikosa na kwa wale waliopata, nashukuru na kumwambia Rais aendelee kufanya yale yamebaki. Pia, namshukuru Rais kwa kufanya Nakuru iwe Mji Mkuu. Hii inamaanisha kuwa hata sisi tunaotumia barabara hiyo, tutasema kuwa tuna mji mkuu katika eneo hilo. Asante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ya kuunga mkono Hotuba ya Rais."
}