GET /api/v0.1/hansard/entries/1133940/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1133940,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1133940/?format=api",
"text_counter": 175,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kwanza, nimesimama kuunga mkono Ripoti ama Hotuba ya Rais ya jana ambayo tuliketi hapa tukaiskiza kwa makini. Rais alileta kwetu mambo kadha wa kadha na kutueleza mengi Serikali yake imefanya. Kwanza, ninataka kumpongeza Rais kwa mambo mawili au matatu kwa sababu ya wakati. Kwanza, ni kumpongeza kwa kuwa ameweza kutenda kazi; sana sana ya miundo misingi ya barabara. Kila mahali tunapotembea nchini, tunaona barabara zimejengwa ama zinaendelea kujengwa. Na kwa kweli Serikali imewekeza sana kwa mambo hayo. Wakati barabara ziko sawa kila mahali, uchumi unaenda mbele kwa sababu wafanyibiashara wanaweza kufanya mambo sawa sawa na wanaotafuta huduma za hospitali wanaweza kuzifikia na kupata madawa kwa wakati ufaao"
}