GET /api/v0.1/hansard/entries/1133942/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1133942,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1133942/?format=api",
    "text_counter": 177,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Tunashukuru Serikali. Kila mahali nchini tumeona kazi ikifanyika. Na kwa kweli, hata kama zile kazi kubwa zinafanyika katika miji mikubwa, hata kule vijijini hatujasahaulika. Ninataka kumshukuru Mhe. Rais kwa maana kule Taita Taveta, Eneo langu la Bunge, mwezi uliopita Waziri wa Barabara alikuja na akaanzisha barabara ya shilingi bilioni mbili nukta mbili. Ni barabara ambayo tumeililia kwa muda mrefu. Lile tunaenda kuomba Serikali ni kwamba kila wakati kazi hizo zinapofanyika katika kiwango cha taifa, serikali za kaunti zisiingilie kati kazi hiyo inayofanywa na Serikali ya taifa. Kwingine tunawaona wale magavana wanasema wao ndio wamefanya hili ama lile. Lakini kama Wajumbe waliochaguliwa kuketi katika Bunge la taifa, kazi zinazofanywa na serikali kuu ni zile sisi tunafanyia oversight. Ningependa kuunga mkono ama kufurahia hali ya usalama nchini. Wanajeshi wetu wamezidi kuajiriwa na kuangaliwa na Serikali. Rais alisema jana hata mishahara yao ziliongezeka. Kuna jambo moja ningependa kulisema na itakuwa vizuri niliseme hapa; jeshi, polisi na vitengo vyetu vya usalama wanapochukuwa watu, bado kuna mambo fulani itabidi waangazie sana. Unakuta maelfu ya vijana wanajitokeza kwenda kwenye recruitment . Lakini, wanaochukuliwa katika kata ndogo ama wilaya ni watu wachache. Utakuta vijana, tuseme, elfu moja wameenda pale, lakini baada ya kupigishwa mbio, kurushwarushwa hapa na pale na kufanyiwa mambo mengi, ifikapo mwisho, ni watu watano tu wanaochukuliwa. Kwingine kama kule kwangu Wundanyi, juzi kulikuwa na aibu sana. Kina dada wetu walizungushwa, wakakimbizwa na kufanyishwa mambo mengi. Baada ya hayo yote, walisema hawatachukua kurutu msichana. Walichukua kadeti mmoja ilhali wale wasichana walijitokeza kwa bidii yote ili wapate nafasi ya kutumikia nchi yao. Kwa hivyo, Serikali lazima itafute mbinu mbadala ya kusajili vijana wetu kuliko kuwafanyisha kazi ambayo haina malipo. Mwisho, ninataka kuongea kuhusu Kazi Mitaani. Aliongea sana juu yake. Alisema kuwa kila kaunti nchini itapata nafasi. Lakini ukweli usemwe: kuna kata ndogo zinazojulikana ni za mashambani ambazo hazina slums . Ukiingia kwenye mtandao, hizo kata ndogo zitakosekana. Wundanyi, ninakosimamia, pekee katika kaunti nzima, haiko katika Kazi Mitaani. Tumefuatilia suala hili na tunaamini kwamba Serikali itaweka Kazi Mtaani katika kila kata ndogo ili vijana wetu wapate kunufaika na pesa ambazo zitawasaidia kukimu maisha yao. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}