GET /api/v0.1/hansard/entries/1134360/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1134360,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1134360/?format=api",
    "text_counter": 166,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ningependa kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na ndugu yangu ‘ landlord .’ Amegusia mambo ya kuharakisha kuinua uchumi, yaani economic recovery, katika lugha ya Kiingereza. Katika Kaunti ya Kilifi tuko na maeneo ya Export Processing Zones (EPZ). Haya ni maeneo ya biashara za nje. Hivi karibuni, tumeona kwamba kampuni za EPZ zimeingia kwa wingi katika kaunti yetu. Zingine hata ziliwacha kufanya biashara zao katika Kaunti ya Mombasa na kwenda Kilifi. Hii ni kwa sababu ya nafasi ya kufanya biashara hizo na wanaweza kupata afueni ya kulipa kodi. Bi. Naibu Spika, Mombasa na Kilifi haziko mbali. Wengi wa watu wanaofanya kazi Kilifi wanaishi Mombasa na wengi wanafoanya kazi Mombasa wanaishi Kilifi, hususan maeneo kama Mtapwa, Majengo ya Kanamahi, Mpingo na Sheriani. Ni maeneno ambayo ina wakaazi wengi wanaoishi kaunti hizi mbili. Jambo la kusikitisha ni kwamba wafanyikazi wa biashara hizo katika maeneo ya Mtwapa wanalipwa pesa duni. Wanafanya kazi katika miji kama vile Mombasa, Nairobi, Kisumu and Nakuru na wanalipwa mishahara ya juu. Bi. Naibu Spika, ndugu yangu katika Hoja hii angesema ikiwa watu wana masaa 24 ya kukuza uchumi kwa njia ya kufanya biashara kama Kilifi na Mtwapa, basi walipwe sawia na wafanyakazi wa Mombasa, Kisumu, Nakuru na miji mingine ambapo kuna maeneo ya kufanya biashara ya nje. Wakati huu, kumekua na ugonjwa wa COVID-19. Watu wamepoteza kazi zao. Hivi karibuni, kumeingia ugonjwa wa Omicron na watu wanazidi kupoteza kazi. Serikali ingekuwa imeweka mikakati kambambe ili kuhakikisha kuwa ugonjwa huu hautaenea kwa kasi kama ule wa COVID-19 ulipotangazwa mara ya kwanza. Wangeangalia ni vipi tunaweza kupata suluhisho ya ugonjwa huu. Tuzidishe upande wa teknolojia kuona kwamba watu wanaweza kufanya kazi zao wakiwa nyumbani ama wanafanya kazi zao wakiwa kwa umbali, lakini wasipoteze kazi. Bi. Naibu Spika, tukija upande wa pesa zinazoenda katika Serikali za mashinani, tunaona ya kwamba bidii ama juhudi katika kupunguza yale madeni ambayo yanakumba serikali za mashinani hazitoshi. Ni jambo la kusikitisha ni kuwa kati ya serikali zetu za ugatuzi zote 47, hakuna serikali hata moja ambayo haina shida ya kutolipa madeni. Wengi wamekuwa wakifanya harakati zao katika serikali zao lakini madeni ya kaunti yanaendelea kupanda kila uchao. Hili si jambo ambalo linaonyesha picha nzuri. Bi. Naibu Spika, tukiangalia upande mwingine, madeni yale ya kulipa yanalipwa kwa kupendelea. Wakati mwingine, wengine wanalipwa na wengine hawalipwi. Watu wamechukua madeni. Hivi sasa, wamekwenda kwenye benki wakachuka na kukopesha kila mahali. Lakini pesa zikipatikana zinapokwenda katika serikali za mashinani, hazigawanyi kulingana na ratiba; kwamba, wale watu ambao wamefanya kazi kwanza walipwe halafu wale wengine baadaye. Kunakuwa na mapendeleo. Kuna wengine ambao wamefanya zile kazi na wameweza kupeleka risiti zao na kupitishwa kwamba wameshalipa yale madeni. Lakini utaona kwamba wale wanaolipwa katika zile pesa zinazopatikana kwenda katika serikali za mashinani wanaanza kufanya ubaguzi. Wale ambao wako na madeni madogo madogo hususan nikigusia wale ambao"
}