GET /api/v0.1/hansard/entries/1134362/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1134362,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1134362/?format=api",
"text_counter": 168,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "wanafanya biashara ndogo ndogo, wamejikakamua sana kufanya hiyo biashara lakini ikifika saa ya malipo inachelewa. Bi. Naibu Spika, sasa utapata kwamba mtu amemaliza karibu mwaka mzima. Anaenda kwa kaunti kila siku akiomba kwamba deni langu katika benki linazidi kupanda na upande huu sasa sijui hata faida hakuna tena, niregesheni ile pesa ambayo nilikopa ili kuwafanyia kazi kama kaunti. Jambo kama hilo ni muhimu lingekuwa hapa na lizingatiwe, kwamba wale wanaofanya biashara na kaunti, wa kwanza walipwe kwanza na watakao kuja baadaye walipwe baadaye, badala ya kufanya mambo ya upendeleo. Tumeona katika Ripoti hii pia kwamba kuna uzembe mwingi sana ndani ya mashirika ya umma. Ndugu yangu Sen. Kibiru amefanya vizuri kuyataja yale mashirika. Shirika la kwanza likiwa ni Kenya Power Company (KPC); shirika la pili likiwa ni Kenya Electricity Generating Company (KenGen); la tatu likiwa ni Kenya Ports Authority (KPA) na la nne likiwa ni Kenya Airways (KQ). Bi. Naibu Spika ni jambo la kusikitisha kuona Serikali yetu inapeleka pesa nyingi sana katika makampuni haya. Kulingana na ukweli, kama mashirika ya umma, makampuni haya yanatakikana kujiangalia wao wenyewe bila kusaidiwa na Serikali. Yawe yanaweza kufanya biashara na wanapata pesa za kujiendeleza wao wenyewe ili waweze kupanuka kama wale wa Emirates Airline, Qatar Airways na KLM Royal Dutch Airlines. Haya ni mashirika ambayo yako kwa serikali zao lakini yanajitegemea na yako huru na Serikali. Lakini hapa utaona kwamba shirika kama KQ linasikitisha. Ni shirika letu la ndege, tunalipenda na kulitumia sana sisi waheshimiwa hapa. Lakini utaona kwamba bei za KQ ni ghali sana. Huduma zake sio mbaya lakini ikiwa huduma zenu zitakuwa sio mbaya lakini kima kile wanaosafiri wanalipa kitakuwa juu kuliko wengine, KQ wanaanza kupoteza biashara. Hii ni kwa sababu sasa tuko na mashirika kama 748 Air Services, Jambo Jet, Skyward Express, na wengineo ambao wanafanya biashara kama hiyo. Uzembe ambao unatokea ndani ya KQ ni lazima urekebishwe ili shirika hili liweze kushindana na hata mashirika ya ndege ya mataifa mengine. Bi. Naibu Spika ukiangalia hivi sasa, KQ haiwezi kushindana na watu kama Emirates kwa sababu bei yao ni kama nusu kama unaenda ama unatoka Dubai. Ukisafiri na Emirates utalipa nusu ya ile nauli ambayo mtu ametumia KQ kutoka Dubai akija Nairobi ama kwenda Dubai analipa nusu. Hiyo ni lazima iangaliwe. Shirika kama la KPA halingekuwa na madeni. Mashirika yote ya bandari, hata ukienda Singapore na Dubai, ndio husaidia serikali. Lakini sisi leo serikali lazima iangalie vile inawezakusaidia KPA. Ni kwa sababu ya uzembe na ufisadi kule. Bi. Naibu Spika, la mwisho ambalo ningependelea kulitaja ni madeni ya barabara. Sisi katika Kaunti ya Kilifi, serikali imejaribu kufanya barabara kisawa kwa uwezo walionao. Lakini tukija katika Serikali ya kitaifa, ni jukumu la Serikali kuona kwamba wanatengenezea wananchi barabara ili waweze kuongeza biashara na uchumi hususan kwa wale wafanyibiashara. Mara nyingi sana utaona kwamba ikiwa Serikali inafikiria kutengeza barabara ndani ya Pwani au pahali popote ambapo inafikiria kutengeneza barabara, kitu cha kwanza kinachokuja kwenye akili ya mtu aliye ndani ya serikali ni kwamba"
}