GET /api/v0.1/hansard/entries/1134364/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1134364,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1134364/?format=api",
    "text_counter": 170,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "tunatengeneza barabara ya kusaidia watalii. Sisi tumechoka na habari ya kwamba ukifikiria kwenda Mombasa, Kwale, Kilifi, Taita-Taveta, Lamu au Tana River unafikiria utalii. Usisahau kwamba kule kuna binadamu. Maeneo ya Pwani sio ya utalii pekee yake. Pwani sio mbuga za nyika ya kwamba kunaishi wanyama. Bi. Naibu Spika, tunataka heshima ifanywe. Ikiwa wewe unaishi kule Pwani na Serikali imefikiria na kutafakari kutengeneza barabara, watengeneze kwa sababu wanajua kuna wakulima, wafanyibiashara, watu wanaishi kule, kuna shule na kila kitu kiko kule. Lakini tunaona kwamba upande wa barabara Serikali imekaba pesa kidogo kwa sababu ya uhaba wa barabara nzuri kule Pwani. Hivi juzi, tumepoteza watu 18 katika ajali ya matatu iliyotokea. Ni mahali ambapo tusingepoteza watu kama hao. Watu wanaoishi kule pia wanahitaji huduma za Serikali. Watu wa Kilifi wanahitaji huduma za Serikali ili wapate barabara nzuri na tusiwe na ajali zinazotokea barabarani na kuweza kupoteza maisha ya wapendwa wetu. Bi. Naibu Spika, la mwisho ni kwamba ndugu yangu “landlord” ameleta Ripoti yake hii na ninaiunga mkono kwa sababu ni safi na imetupatia nafasi ya kuangalia vigezo vile ambavyo tunaweza kuongeza uchumi. Asante."
}