GET /api/v0.1/hansard/entries/1134384/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1134384,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1134384/?format=api",
"text_counter": 190,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bi. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Ripoti ya Kamati ya Fedha na Bajeti ya Bunge la Seneti kuhusiana na taarifa ya sera ya bajeti ya mwaka 2022/2023. Kwanza, naipongeza Kamati hii kwa kuiangalia kwa kikamilifu taarifa hii ya sera kulingana na Kanuni ya Seneti na Katiba yetu ya Kenya. Taarifa hii inatupa mtazamo wa vile Bajeti ya mwaka ujao itakavyo kuwa katika maswala yote ambayo yameangaziwa katika sera hiyo. Bi. Naibu Spika, pili, nakubaliana na mapendekezo ya Kamati hii kwamba hazina kuu ifanye makerebisho ili kuzikinga kaunti zetu dhidi ya mfutuko wa bei au inflation na kwamba ruzuku ya mwaka ujao wa 2022/2023 iongezeke kwa asili mia 35 ya hesabu za serikali za mwaka wa 2017/2018. Hizo ndizo audited accounts au hesabu ambazo zimekaguliwa na mhasibu mkuu wa serikali ambazo ndizo za mbele zaidi kuliko zingine zozote. Serikali Kuu inafaa kutumia asili mia 35 za fedha hizo ambazo ni karibu Kshs1.4 trillion. Asili mia 35 ni moja ya vitu ambavyo vilikuwa katika BBI. Rais Uhuru Kenyatta alipohutubia Bunge mwanzo wa mwezi huu, alisema kwamba BBI bado ipo hai ijapokuwa imewekwa katika freezer kwa sasa kutokana na uamuzi wa mahakama. Natoa changamoto kwa Serikali kwamba kama kweli ina nia, inafaa kuonyesha nia hiyo. Kwa sasa, inafaa kuwapa kaunti zetu asili mia 35 ya fedha zote ambazo ni karibu Kshs1.4 trillion. Ikiwa Serikali Kuu haitafanya hivyo, inamaana kuwa mapendekezo ya BBI yalikuwa ya kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Bi. Naibu Spika, naunga mkono pia pendekezo la kuongeza ruzuku ya kaunti kutoka Kshs370 bilioni mpaka Kshs495 bilioni. Ikiwa pendekezo hilo litakubalika, Kaunti ya Mombasa inanuia kupata karibu Kshs12 bilioni ambazo ni pesa zinazohitajika pakubwa katika kutoa huduma kwa wakaazi wa Mombasa na wengine wanaozuru Mombasa. Jambo lingine lililogusiwa ni sekta ya usafiri. Ninaposema usafiri, namaanisha usafiri wa meli na wa bahari. Ijapokuwa Serikali inaweka pesa nyingi katika kujenga viwanja vya ndege, barabara pia zinahitajika. Kwa mfano, miaka miwili iliyopita, Serikali ilitenga karibu Kshs8 bilioni katika kupanua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi ilioko Mombasa. Lakini ndege za kimataifa zinazotua Mombasa ni moja au mbili tu. Zamani, ndege za Turkish Airlines, Qatar Airways, Ethiopia Airlines pamoja na ndege zingine za kibinafsi zilikuwa zinakodishwa kuleta watalii katika kaunti za Pwani. Lakini kwa sasa, ndege ya kimataifa inayotua Mombasa ni Ethiopian Airlines pekee yake. Bi. Naibu Spika, tunataka kuinua uchumi wetu baada ya kuathirika na janga la COVID-19 lakini hatuwezi kuinua uchumi wa utalii wakati tunazuia ndege za kimataifa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi ulioko Mombasa au katika Uwanja wa ndege ya Malindi ambayo pia iko katika hali ya kimataifa. Haina faida kutoa Kshs8 bilioni kurekebisha uwanja wa ndege wa Moi ulioko Mombasa wataki kwa sasa, ndege inayotua huko ni ile ya Ethiopia Airlines pekee yake. Tukilinganisha Pwani yetu ya Kenya na nchi jirani kama Zanzibar, wanatushinda kwa mbali. Kisiwa cha Zanzibar kinapokea zaidi ya ndege 30 za kimataifa kila wiki."
}