GET /api/v0.1/hansard/entries/1134386/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1134386,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1134386/?format=api",
    "text_counter": 192,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Kuanzia Jumatatu hadi Jumapili, ukienda katika Uwanja wa Kimataifa wa Zanzibar, utapata ndege nyingi za kimataifa kama Qatar Airways, Emirates Airways, na vile vile, ndege nyingi za kutoka Europa ambazo zinawasafirisha watalii moja kwa moja hadi Zanzibar. Kupatikana kwa ndege hizo za kimataifa kumeinua sana uchumi wa Kisiwa cha Zanzibar. Bi. Naibu Spika, nina ushahidi kamili kwamba zamani Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi ulioko Mombasa ulipojengwa ndege zote za kimataifa zilikuwa zinatua Mombasa. Ndege za kimataifa kama Lufthansa, Air France, British Airways, Condor Airlines na zingine nyingi zilikuwa zinaleta watalii mara kwa mara ili kuinua biashara ya utalii. Ni jambo la aibu kwamba leo Mombasa ina bandari ya kimataifa, kwani kunajengwa hata Cruise terminal ambayo itatumika na watalii wanaowasili nchini kwa meli. Ingekuwa ndege za kimataifa zinaruhusiwa kutua Mombasa, watalii wengeweza kuja kwa ndege na hata kurejea kwa meli. Vile vile mtalii angeweza kuwasili nchini kwa meli na kurejea kwa meli au ndege. Hili likitimizwa, litainua zaidi uchumi wetu na biashara zetu za kitalii katika Kaunti ya Mombasa na kaunti jirani. Bi. Naibu Spika, kuna uwanja wa ndege wa kimataifa Kisumu pia lakini ndege inayotua huko ni Kenya Airways tu; hata ndege ya 540 haitui Uwanja wa Kimataifa ilioko Kisumu. Tutaendelea kuilinda Kampuni ya Ndege ya Kenya Airways hadi lini? Kampuni ya Kenya Airways inaendelea kupata hasara. Kila mwaka, mabilioni ya fedha yanakwenda kwa hasara. Jambo la kushangaza ni kwamba kuna waekezaji wa kibinafsi ambao wako katika Kenya Airways lakini wakati pesa zinahitajika, Serikali ya Kenya tu ndio inayotoa pesa. Kodi zetu pekee yake ndizo zinatumika kuinua Kenya Airways. Waekezaji wa kibinafsi huwa hawaongezi mtaji wakati Kenya Airways inaendelea kupata hasara. Ikiwa tunaweza kuruhusu meli za kimataifa kuegesha Mombasa na kuleta mizigo, sioni ni sababu gani ndege za kimataifa haziruhusiwi kwenda Mombasa kuleta watalii ili kuinua sekta ya utalii Mombasa. Tuna fuo za bahari nzuri sana kutoka Shimoni hadi Kiunga, Lamu, lakini hakuna ndege za kimataifa zinayotua katika sehemu hizo. Mbali na ufuo wa bahari, tuna mbuga za wanyama kama Tsavo na zinginezo ambazo ni vituo vikubwa vya kimataifa kwa maswala ya utalii. Bi. Naibi Spika, vile vile, Bandari ya Lamu ambayo ni ya kimataifa, bado haijaweza kuanza kazi kikamilifu. Serikali kuu inafaa kupeleka waekezaji wa kibinafsi kule Lamu ili biashara ianze kuwa katika Lamu. La sivyo, bandari ya Lamu itakuwa"
}