GET /api/v0.1/hansard/entries/1134390/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1134390,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1134390/?format=api",
    "text_counter": 196,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "isiwachiliwe kufa kifo cha kawaida kwa sababu hiyo ni njia moja ambayo pesa za serikali zinaliwa bila kuchunguzwa na mhasibu mkuu wa Serikali ya Kenya. Hivi majuzi, tulipata habari kwamba kuna meli moja ambayo imebeba mabaki ya sumu ya nuclear kutoka Ulaya zinazokuja kutupwa Afrika. Kufikia jana ripoti zilikuwa kwamba meli hiyo ilikuwa imewasili katika Bandari ya Mombasa. Naomba Serikali ihakikishie nchi kwamba meli hiyo itasafirishwa na Navy ya Kenya mpaka bahari kuu ili kuhakikisha kwamba mabaki hayo ya sumu hayatupwi nchini kwetu na kutuletea madhara. Mabaki hayo ya sumu kule Ulaya yanachunguzwa na Greenbelt Movement lakini hapa Kenya, sisi hatuna vifaa au tajriba ya kuhakikisha kwamba vitu kama hivi haviwezi kutupwa hapa. Ni muhimu Serikali ituhakikishie sisi wananchi wa Kenya kwamba mabaki hayo ya sumu hayataweza kutua kokote katika nchi ya Kenya au mahali pengine. Bi. Naibu Spika, jambo lingine ambalo nimeangaziwa ni maeneo ya biashara nje au Export Processing Zones (EPZs) hususan ilioko Mombasa katika Dongo Kundu. Mwaka jana, nilijumuika na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Bajeti, Sen. Kibiru, kuzuru eneo hilo. Isipokuwa mradi huo uliwekewa jiwe la msingi katika mwaka wa 2019, mpaka sasa, hakujakuwa na maendeleo yoyote. Squatters hawajaondolewa na vile vile, hakuna waekezaji ambao wametafutwa ili kuwekeza na kuinua biashara katika Kaunti ya Mombasa na Kenya kwa jumla. Dongo Kundu EPZ itasaidia pakubwa kuinua uchumi wa Mombasa na pwani na vile vile kupata mapato zaidi ya serikali kwa sababu ni sehemu ambayo iko tayari. Waekezaji wanafaa tu kuitwa ili wajenge viwanda na kuhakikisha kwamba biashara inaendelea ili sisi watu wa Mombasa na majirani zetu wa Kwale na Kilifi waweze kufaidifka na biashara hizo. Bi. Naibu Spika, Serikali imesema itajenga hospitali 50 za Level 3 . Kulingana na taarifa iliyosomwa na Rais alipokuja Bunge, alisema kwamba wamejenga hospitali 20 katika Kaunti ya Nairobi kwa mwaka mmoja. Hizi ni hospitali chache kwa sababu kuna sehemu ambazo hazina hospitali ya aina yeyote. Wengi wao wanatumia dawa za kienyeji na miti shamba. Kwa hivyo, hospitali hizi zinafaa kujengwa kwa kila kaunti ambazo kwa sasa ziko na shida ya huduma za afya wakati huu tuko na janga la Coivid-19. Bi. Spika wa Muda, ninapomalizia, ninaipongeza Kamati kwa kazi nzuri waliyoifanya. Tunasisitiza kwamba afisa mkuu msimamizi wa maswala ya pesa azingatie mapendekezo ambayo yametolewa na Kamati hii ili kuhakikisha kwamba Kamati au Bunge la Seneti hazichukuliwi kama rubber stamp na kufanyiwa kama ada lakini yale yaliyo pendekezwa nakushauriwa na Kamati hii ya Fedha hayatazingatiwa. Ni muhimu wazingatie na tuhakikishe kwamba Bunge la Seneti linachukuwa sehemu yake katika taasisi za kitaifa zinazoangalia mambo kwa undani na kuhakikisha usawa unatendeka."
}