GET /api/v0.1/hansard/entries/1135640/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1135640,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135640/?format=api",
    "text_counter": 179,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante Bi. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ningependa kuwatolea shukurani sana ndugu zangu Maseneta wenzangu kwa kushughulika sana na shughuli za Bunge. Tumekuwa pamoja mwaka huu mzima; tunashukuru Mungu tumefika mwisho. Tuna jambo la kushukuru sana Mwenyezi Mungu. Pili, ningependa vile vile kuwashukuru sana Maseneta, kwa ukakamavu waliokuwa nao mwaka mzima. Tumeweza kufanya bidii kuhusiana na Bills na Motions . Kuna kazi nyingi sana ambazo tumeendelea nazo, ambazo hata rekodi yake iko na inaweza kuonekana. Kwa hiyo, nataka kuwapatia kongole ya hali ya juu sana Maseneta wote walioko hapa na wale ambao wako katika nyadhifa mbalimbali. Hawakuweza kufika lakini juhudi zao tumeziona na tunashukuru sana. Bi. Naibu Spika najua si kitu rahisi sana kuwa ndani ya Bunge na kuchukulia hatua safari mbalimbali kuweza kuweka mambo ya Bunge la Seneti kwa hali ya juu. Ndio sababu ukaona ndani ya hili Bunge la Seneti, kuna watu ambao ni wakakamavu na wanajulikana. Ukitaka sekta zote za Wakenya ziko hapa. Tuna watu wa hesabu, sayansi, mawakili, wafanyabiashara na watu wa sehemu mbalimbali. Kwa hivyo, wote hao wamekuwa wakichanganya maoni yao kuleta hapa ndani ya Seneti. Vile vile, tumekuwa na wema. Hatukuweza kutupiana maneno hapa ama kukosana na kushambuliana vibaya. Sote tumekuwa ndugu moja tukifanya kazi kusaidia Wakenya kokote walipo ndani ya Serikali yetu ya Kenya. Kwa hivyo, nataka kuwashukuru sana. Bi. Naibu Spika, mwisho ni kuwatakia kila la kheri. Najua kutakuwa na shamrashamra nyingi za Krisimasi na kutakuwa na starehe nyingi sana ambazo zitakuja wakati wa mwaka mpya, ambao tutakuwa tunafungua. Ingekuwa vyema kuwaambia tu ndugu zangu kwamba zile shamrashamra na harakati zote tutakazokuwa nazo wakati wa Krisimasi na mwaka mpya, tuziangalie vizuri na tuzingatie maoni yale ya Wizara ya Afya--- Tuketi mbalimbali tuweze kujikinga na ugonjwa huu wa COVID-19 ama huu mwengine umekuja ukaingilia katikati unaitwa OMICRON."
}