GET /api/v0.1/hansard/entries/1135642/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1135642,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135642/?format=api",
"text_counter": 181,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Najua umefika hapa kwetu, lakini najua Wakenya ni watu ambao wanaelewa wakiambiwa kitu. Kwa hivyo, jukumu letu kama Seneti ni kuwaambia Wakenya popote walipo wazingatie zile amri za Wizara ya Afya; ya kwamba tuweze kujitenga na kuvaa barakoa wakati tunaongea na wenzetu ili huu ugonjwa usiweze kutapakaa ndani ya nchi yetu ya Kenya. La mwisho kabisa ni kwamba afya njema panapo majaliwa Mwenyezi Mungu atakapopenda tuonane tena - vile hapa katika shughuli zetu za Bunge tunasema “kesho” - tukiwa tutafungua Bunge vyema sote tuwe salama kwa amri yake Mwenyezi Mungu na rehema zake. Asante, Bi. Naibu Spika."
}