GET /api/v0.1/hansard/entries/1135648/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1135648,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135648/?format=api",
    "text_counter": 187,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cherargei",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13217,
        "legal_name": "Cherarkey K Samson",
        "slug": "cherarkey-k-samson"
    },
    "content": "Nina mambo mawili. Kwanza, ni kuwauliza Wakenya wachukue tahadhari haswa wakati huu wa sikukuu. Waendeshaji magari wasafirishe Wakenya kwa njia ya utaratibu ndio tusikuwe na ajali za barabarani wakati huu wa msimu wa Krismasi. Wale wanaotoka sehemu za Magharibi mwa Kenya wamepata gari la moshi jipya ambalo linaelekea sehemu hio. Tunatarajia ya kwamba itarahisisha kusafarisha wakaazi ambao wengi wao wanatoka Magharibi mwa Kenya, ingawa gari la moshi hilo linaenda kwa mwendo wa mzee kobe. Tunatarajia Shirika husika la Reli nchini litaangalia mahali ambapo gari la moshi linapita. Jana tuliona kulikuwa na mshike mshike kidogo, lakini tunatarajia Shirika la Reli nchini litaweza kushughulikia na kuhakikisha tunasafiri kwa njia inayofaa. Bi. Naibu Spika la mwisho ni kwamba Wizara ya Afya imesema kwamba Wakenya ambao hawajapata chanjo ya Covid-19 hawatapata huduma za serikali. Wizara ya Afya ilikuwa imeahidi ya kwamba Wakenya millioni kumi watakuwa wamepata chanjo kufikia mwisho wa mwaka. Lakini, kwa sasa, hicho kiwango hakijafika. Kwa hivyo, Wakenya wanapotarajia kupata chanjo, pia Wizara ya Afya ihakikishe kuwa chanjo hizo zinapatikana hadi kule mashinani ndio iwe rahisi kuzipata. Bi. Naibu Spika, tunapomaliza mwaka ninawatakia kila la heri wenzangu. Najua tunaelekea mwaka wa uchaguzi lakini cha muhimu ni taifa letu liwe la wapenda amani. Baada ya Mwezi wa Tatu au Nne, vyama vingi vitaelekea mchujo. Ni vizuri kwa sababu kinara wa chama, Sen. Wetangula, yuko. Kwa hivyo, ataweza kupeleka jambo hili kwa vinara wa vyama wahakikishe mchujo ambao unafanyika mwaka ujao utakuwa wa huru na haki. Asante Bi. Naibu Spika, kwa nafasi hii."
}