GET /api/v0.1/hansard/entries/1135650/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1135650,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135650/?format=api",
    "text_counter": 189,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. M. Kajwang’",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13162,
        "legal_name": "Moses Otieno Kajwang'",
        "slug": "moses-otieno-kajwang"
    },
    "content": "Bi. Naibu Spika, ningependa kuwashukuru Maseneta wenzangu kwa kujitolea katika kazi hii ya ujenzi wa taifa. Kuna wale ambao wanadhani ujenzi wa taifa ni kujenga barabara, nyumba au reli. Lakini, taifa linaweza kujengwa kwa sera na sheria ambazo tunapitisha. Ningependa kuwapongeze na kuwashukuru wenzangu kwa sababu kuna sheria mbili ambazo nilileta hapa Seneti na leo zimepitishwa na tunangojea tu kuzipigia kura. Sheria ya kwanza inapendekeza kwamba viongozi katika kila kaunti wawe na kongamanona, wawe wakikutana ili wajadiliane kwa yale maneno ambayo yanahusu hizo kaunti. Mkikumbuka Waheshimiwa Maseneta, sheria kama hio tuliipitisha kwa Seneti ama Bunge la 11. Lakini, Magavana walikimbia kortini. Sasa, tunatumaini ya kwamba tutapata fursa ya kuketi na magavana na wale viongozi wengine ambao wamechaguliwa kutoka kaunti zetu ili tujadiliane."
}