GET /api/v0.1/hansard/entries/1135653/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1135653,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135653/?format=api",
    "text_counter": 192,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. M. Kajwang’",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13162,
        "legal_name": "Moses Otieno Kajwang'",
        "slug": "moses-otieno-kajwang"
    },
    "content": "Tumeona pale Nairobi Kaunti kuna Nairobi Metropolitan Services (NMS) ambayo imepewa mamlaka na madaraka mengine ambayo yalikuwa ya Kaunti ya Nairobi. Nawashukuru wenzangu kwa kuipitisha hio pia. Sheria ya tatu iliyopitia Kamati ya Ugatuzi na Mahusiano kati ya Serikali za Kaunti na Serikali kuu ililetwa na Sen. OleKina. Ni sheria ambayo inaashiria na kuhimiza serikali za kaunti wafanye na waweke sehemu za public participation. Bi. Naibu Spika, leo hii nilijitolea niwe hapa. Hii ni kwa sababu leo hii kuna mwalimu ambaye ni maarufu sana kule kwetu Karachuonyo anaitwa Koyo Orimbo ilikuwa inafaa niende nimuomboleze. Kuna mama ambaye watoto wake wamejitolea kabisa. Kijana wake anaitwa Julius Olumbe kule Suba Kaskazini na ilikuwa nafaa niende nimuomboleze. Kuna mzee rafiki yangu ambaye anaitwa Kennedy Osutswa ambaye kijana wake alikuwa mwanafunzi akisomea uhandisi chuo kikuu. Aliuawa kinyama. Bado tunahimiza Serikali na Directorate of Criminal Investigation (DCI) wafanye uchunguzi mwafaka, ilikuwa inafaa niende nimuomboleze. Kuna mamake rafiki yangu Harold Ochola ambaye ilikuwa pia nafaa nimuomboleze. Mbali na mazishi hayo, ilifaa mimi kama kijana niwe na mama, watoto wangu na familia. Kwa hivyo, hio ni kujitolea. Ninajua kila Seneta hapa amejitolea. Ningependa nichukue fursa ya mwisho kuwatakia Krismasi mwafaka na mwaka mpya ulio na manufaa. Tunajua hii Desemba itakuwa ya mwisho kwa Bunge la Kumi na Mbili. Kwa hivyo, naombea kila Seneta yule ambaye atataka kuwa gavana, yule atarudi hapa na ambaye atataka kuwa rais kama mkubwa wangu, Sen. Wetangula. Tunawatakia kila la kheri na tunahakika ya kwamba taifa letu la Kenya lastahili heshima na hio heshima tutapata kwa uchaguzi ambao unakuja. Asante sana, Bi. Naibu Spika."
}