GET /api/v0.1/hansard/entries/1135665/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1135665,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135665/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Musuruve",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13188,
        "legal_name": "Getrude Musuruve Inimah",
        "slug": "getrude-musuruve-inimah"
    },
    "content": "Asante sana Bi Naibu Spika kwa kunipa fursa hii ya kuchangia Hoja hii. Nawashukuru maseneta wenzangu kwa kazi tuliyo fanya mwaka huu. Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tumeweza kuunda sheria ingawa pia kuna zingine ambazo hazijakamilika. Ni jukumu letu kuendelea kuunda sheria bila kuchoka. Ninajua kwamba wakati tutarejea vikao vya Seneti mwaka kesho, tutajikakamua kuja hapa na kuzungumzia mambo ya sheria kwa sababu waKenya wanatusubiri na wanataka kuona tunawatetea. Seneti inajukumu la kutetea wakenya na hiyo ndiyo kazi yetu. Nawaahidi walemavu kwamba sitachoka; nitaendelea kuwatetea hapa Seneti. Ninashukuru Seneta wenzangu kwa sababu nikizungumzia maslaha ya walemavu huwa wanajiunga nami na tunaweza kuhakikisha walemavu wamepata haki yao. Tutaendelea kuzungumza kuhusu sheria ya lugha ya ishara. Nataka kuwahakikishia walemavu katika nchi yetu ya kuwa nina imani Maseneta wenzangu watajiunga nami na watahakikisha kwamba sheria ya lugha ya ishara imepita kikamilifu na pia kupelekwa katika Bunge la Kitaifa. Ni ombi langu kuwa Mswada huo utakapo fikishwa katika Bunge la Kitaifa, hautachelewa na Rais ataweza kuweka muhuri uwe sheria rasmi. Najua kuwa walemavu wamekuwa na changamoto kwa sababu kuna mambo mengi sana ambayo hayajawekwa kisheria. Sen. (Dr.) Mwaura, pia aliwasilisha Mswada mwingine unaolenga walemavu unajadiliwa na tunaomba kuwa utakuwa sheria kamilifu ili walemavu wapate haki yao."
}