GET /api/v0.1/hansard/entries/1135667/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1135667,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135667/?format=api",
"text_counter": 206,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Musuruve",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13188,
"legal_name": "Getrude Musuruve Inimah",
"slug": "getrude-musuruve-inimah"
},
"content": "Bi. Naibu Spika, wakenya lazima wajue kwamba tunaenda likizo lakini tutaendelea kuwa viongozi. Tukiwa likizo, nawaomba Maseneta wazidi kuwasiliana na wakaazi wa kaunti zao. Maswala ambayo hayendelei vizuri mashinani, tuyalete hapa Seneti ili wakenya waishi kwa amani. Ningependa kuwakumbusha wakenya kwamba ingawa tunaenda likizo wanafaa kuwa waangalifu. Huu ugonjwa wa COVID-19 si wa kuchukulia kiholela; ugonjwa huu unaambukiza kina mama, baba na kila mtu. Wakenya wanafaa kuwa waangalifu kwa kuvalia barakoa na kunawa mikono ili ugonjwa huu usiendelee kusambaa. Tunafaa kuchunga maisha ya wenzetu."
}