GET /api/v0.1/hansard/entries/1135672/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1135672,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135672/?format=api",
"text_counter": 211,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen Wetangula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 210,
"legal_name": "Moses Masika Wetangula",
"slug": "moses-wetangula"
},
"content": "Bw. Spika, asante sana kwa kunipa fursa hii kuchangia yale wenzangu wamesema tunapofikia kikomo cha muhula huu wa mwaka huu. Kwanza ni kukushukuru wewe Bwana Spika na kikundi chako, wakiwemo Naibu Spika, Sen. (Prof) Margaret Kamar na wale wenzetu waliomo kwa jopo la Spika na ambao mara kwa mara huchukua nafasi ya kukaa katika kiti chako na kuongoza mijadala ya Seneti hii kwa njia ya heshima na ambayo inastahili sifa. Mwaka huu wote hatujawai kuwa na taharuki yoyote katika Bunge hili; hata wakati ambao tulikuwa tumeganyika kuhusu ugavi wa pesa, ilifanyika kwa njia ya heshima. Kila mtu alitoa maoni yake, ikasikizwa, ikakubalika na ikaheshimimka. Bunge la Seneti limejitenga kama Bunge la kuaminika. Kama ndungu yetu anayewakilisha Kaunti ya Kilifi amsema, Bunge la Seneti lina Maseneta wenye vipaji mbali; tuna maprofesa, mawakili, madaktari na pia mahandisi. Maseneta walioko hapa wanatajriba mbali mbali. Tunapotamatisha vikao vya Seneti vya mwaka huu, tuangazia kule tumetoka, tulipo na tunako elekea na kujivunia kuwa tumepitisha Miswada na Hoja nyingi ambazo zinaleta mabadiliko kwa Wakenya. Jana tulijadiliana kuhusu Budget Policy Statement (BPS) au Sera ya bajeti na kauli kutoka hazina kuu ambayo inahusu bajeti ijayo. Maseneta walichangia hoja hiyo kwa uwazi na wakasema kuwa hata liwe liwalo, eneo za ugatuzi zinahitaji kuongezewa pesa kwani huko ndiko wananchi wa Kenya wanaishi na hivyo wanahitaji kupewa huduma zinazotakikana kwa mfano, matibabu, elimu za chekechea na vitu vingine. Nikimalizia, nawaomba wenzangu katika uwanja wa kisiasa wawe wakarimu wanapoendeleza kampeni. Wakenya wengi watuona sisi wanasiasa kana kwamba tumegeuza uwanja huo kuwa uwanja wa fujo. Nataka kuomba sote tukubaliane"
}