GET /api/v0.1/hansard/entries/1135709/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1135709,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135709/?format=api",
    "text_counter": 248,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Farhiya",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13179,
        "legal_name": "Farhiya Ali Haji",
        "slug": "farhiya-ali-haji"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia mjadala huu. Wacha hata mimi nijaribu leo. Hua napigia Maseneta simu kila siku nikiwaomba wapigie mjadala fulani kura. Nina washukuru sana kwa kuitikia mwito wangu kila wakati. Nina wahimiza Wakenya wachukue chanjo kama wanataka tupigane na Korona na maisha yetu iendelee vile ilikua inafaa kuwa. Serikali inatoa chanjo bure. Watu waende kwenye hospitali na wapewe chanjo. Bw. Spika, nina wahimiza magavana walipe watu pesa ambazo wanandaiwa. Walipe watu wa mashinani pesa ili watu waanze kujiokoa kutokana na umaskini ambao umeletwa na ugonjwa wa Korona. Nina wahimiza Maseneta kuwa Mungu akitujalia tupate fursa ya kukutana hapa tena mwaka ujao, tuta pitisha mijadala mingi. Hii ni kwa sababu tuko karibu kumaliza muhula wa Seneti hii. Tusiwache watu wamefanya bidii wakaleta Miswada hapa Bunge na waende nyumbani bure bilashi bila kupitisha Miswada yao. Ningependa Spika wetu atumie ushawishi wake kuhakikisha kwamba Bunge la Kitaifa lipitishe Miswada yetu ili iwe sheria. Bw. Spika, tuko na fursa nzuri katika historia ya taifa letu kwa sababu tunatengeneza sheria ya kufanikisha ugatuzi. Sheria hizo ni nzuri na ni lazima zipite ili wananchi wapate mafanikio ya ugatuzi. Nina washukuru Maseneta kwa kutetea ugatuzi wakati wowote kulingana na jukumu lao. Ninawasihi Wakenya kuwa watu wanao wania kiti cha urais ni wengi sana. Kila mmoja anajirembesha kuwa yeye ndiye mzuri zaidi. Ninawaomba Wakenya waweke watu ratil ili wahakikishe kwamba yule wanampea mamlaka anafaa kuendesha nchi yetu mbele. Bw. Spika, ninashukuru kila mtu kwa huu mwaka ambao tumemaliza vizuri zaidi. La mwisho ni ningependa kuwatakia Wakenya, Maseneta, sekretarieti na kila mtu ambaye anatusaidia kuendesha shughuliza za Seneti sikukuu njema. Asante, Bwa. Spika."
}