GET /api/v0.1/hansard/entries/1135714/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1135714,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135714/?format=api",
"text_counter": 253,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Milgo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13174,
"legal_name": "Milgo Alice Chepkorir",
"slug": "milgo-alice-chepkorir"
},
"content": "ingawa bajeti hiyo haina pesa za kutosha kuenda mashinani. Inamaanisha kwamba huduma kule mashinani hazitatimizwa kikamilifu, haswa tukiangalia upande wa elimu. Mimi binasfi nimepata kujua kwamba mambo ya wanafunzi kugoma kila wakati ni kwa sababu ya upungufu wa matumizi katika shule na msongamano katika bweni na vyumba vya mamkuli. Ninafikiri kwamba tukiendelea kuongelea haya mambo, Serikali kuu itatuongeza pesa ili mambo kama haya yaweze kuangaliwa ili huduma zipeanwe inavyo stahili. Bw. Spika, msimu huu si wa Krismasi pekee bali pia ni msimu wa siasa. Ningependa kuhimiza Wakenya wenzangu kwamba wakati huu sio wa kuenda kupiga kura mara ya mwisho. Tutapiga kura mwaka wa 2022 na bado tutakuwa na miaka ingine ya kupiga kura. Kwa hivyo, tujitenge na mambo ya kupigana. Lazima tukae tuskize kila mwanasiasa. Kama vile imesemwa, kuna wengi wanawania kiti cha urais. Vile vile kuna wale wawania kiti cha Seneta, Gavana na Wawakilishi Wodi. Tunasahili kukaa na kuskiza hawa kisha tukate kauli bila kupigana. Ni lazima tujue kwamba baada ya ya siasa hawa wakubwa wana salimiana na kunywa chai pamoja. Hatutaki kumwaga damu bila sababu. Bw. Spika, ningependa kutakia Wakenya wote kila la heri, haswa watu wangu wa Kaunti ya Bomet. Wahakikishe kwamba wakati huu wa Krismasi, wajitenge na mambo ya kuchangamka bila kuhakikisha wamefuata maagizo ya Wizara ya Afya. Mbali ya hayo, wahakikishe kwamba wamepata chanjo ya COVID-19. Hii ni kwa sababu hivi sasa kuna aina ya Korona mpya inaitwa Omicron na ni hatari sana. Tayari tuko na chanjo za kutosha katika vituo vya afya na chanjo hazina madhara yoyote. Bw. Spika, la mwisho, ningependa kutakia kila la heri Maseneta wenzangu, Nawatakia Krismasi njema na mwaka mpya wenye fanaka."
}