GET /api/v0.1/hansard/entries/1135719/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1135719,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135719/?format=api",
    "text_counter": 258,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Eng.) Hargura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 827,
        "legal_name": "Godana Hargura",
        "slug": "godana-hargura"
    },
    "content": "Kaunti ya Marsabit. Kwa bahati mbaya kulikuwa na ukosefu wa amani katika Kaunti ya Marsabit na watu wengi wamepoteza maisha yao takriban zaidi ya watu 100. Kuna wakati hesabu ilikuwa ilifanywa. Mali nyingi imeibiwa na nyumba kuchomwa. Ni huzuni sana kwangu kuwakilisha kaunti kama hii katika Seneti. Kila wakati tunajaribu kutatua hali hii na kwa bahati mbaya ni vita na ukosefu wa amani ambao unatokana na viongozi na wanasiasa ambapo mpaka sasa hali haijatulia na haijabadilika. Inaendelea tu kuharibika. Naomba Mwenyezi Mungu tukiwa tunaelekea wakati wa siasa aweze kutupatia njia ya kutatua shida hii. Ni kwa sababu ni wakati ambao tutakuwa na changamoto nyingi sana kwa sababu ya kuchochea watu. Bw Spika, ninawahimiza viongozi wote waliochaguliwa katika Kaunti ya Marsabit katika nyanja mbali mbali ikiwa ni kutoka Members of County Assembly (MCAs) mpaka magavana na viongozi wengine wote ambao pia wanahusika katika hali moja ama nyingine katika katika Marsabit, tukae pamoja tuweze kutatua Hali hii. Viongozi wakikosana haimaanishi kwamba mpaka tuhusishe raia kupatikane vifo na mali kuhalibiwa. Kuna njia nyingi sana ya kutatua tofauti za kisiasa. Nataka kuwashukuru wazee kutoka jamii tofauti za Kaunti ya Marsabit hasa wale 53 ambao walijaribu na bado wanaendelea kuleta amani haswa wale wenyeviti kutoka jamii tofauti wakiongozwa na kijana Jacob Elisha. Wiki mbili zilizopita walikuja Nairobi kwa warsha ya mambo ya amani na wakatutafuta sisi viongozi wakasema ni lazima tuweze kukaa chini. Bw Spika, hakuna kitu kinaendelea katika mji wa Kitale. Biashara zimefungwa, watu wamehama na hata imefika kiwango amri imetolewa hizi piki piki zote zisimamishwe. Sasa uchukuzi umesimamishwa na hali sio nzuri hata kidogo. Mpaka hata jana jioni najua kuna kijana aliuawa. Ni hali ambayo inahuzunisha sana. Wakati wazee hawa walikuja tulikaa nao kama viongozi na tukasema wote wahusishwe. Tukasema tukae kama viongozi na katika mkutano huo, lazima Gavana wa Kaunti ya Marsabit na Waziri wa Fedha wahudhurie kwa sababu tunajua umuhimu wao katika mambo ya jamii huko haswa katika ukosefu wa amani. Tulikaa na tukakubaliana kwamba tutashauriana na watu wetu wasimamishe vita. Leo siku ya Jumatano ingekuwa ni siku tungekuwa na mkutano huo huko Marsabit. Bw Spika, lakini kwa bahati mbaya na kwa sababu ya watu ambao hawataki amani, Jumamosi iliyopita kulitokea mauaji ya zaidi ya watu 13 na mali ikachukuliwa lakini iliweza kurudishwa. Hiyo sasa imevuruga tena ile hali na mpango tulikuwa nayo. Ninataka kuwahimiza wakaazi wa Marsabit watulie na viongozi tuje pamoja bado turudi tuweze kushikana na wazee wetu na kuwahimiza watu wetu wasimamishe vita halafu tuanze taratibu ya kujadili njia ya kuleta amani. Vile ambavyo tumeangalia, hivi ni vita ama ukosefu wa amani ambao unatokana na siasa na ni vitu ambavyo lazima viongozi tukae chini tuweze kutatua. Tumejaribu lakini imeshindikana kwa sababu viongozi wengine hawako tayari kukaa na wenzao na jambo hili linachangia ukosefu wa amani. Bw Spika, pamoja na hayo, nataka pia nielekeze huu ujumbe kwa serikali kuu kwa sababu ni jukumu lao kudumisha amani na kuchunga maisha na mali ya Wakenya wote bila kujali msimamo wao wa kisiasa, jamii au dini. Lazima serikali ihudumie kila"
}