GET /api/v0.1/hansard/entries/1135721/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1135721,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135721/?format=api",
"text_counter": 260,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Eng.) Hargura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 827,
"legal_name": "Godana Hargura",
"slug": "godana-hargura"
},
"content": "mtu kwa usawa. Lakini hali ambayo tunaona kama wakaazi wa Marsabit sivyo serikali inatuhudumia. Serikali pia katika hii vita imeonekana ni kama inaegemea upande mmoja. Jamii fulani ikivamiwa, serikali haina habari lakini wengine wakivamiwa ni tofauti. Juzi ilifika kiwango tuliona mara ya kwanza serikali inakuja na nguvu sana kuhakikisha kwamba jamii fulani ikivamiwa wanafuata wale wengine kurudisha mali yao. Lakini hawa wengine wakati walikuwa wanavamiwa serikali hata ukijaribu kuwaambia wachukue hatua, hawataki kujua. Wana lawama na wajue kwamba serikali ni ya kila mtu na inatakikana ihudumie kila mtu. Bw Spika, katika hii hali ya ukosefu wa usalama kuendelea katika Marsabit mpaka kufika kiwango hiki, yangu ni kusema kwamba hata wao wanachangia kwa sababu ya kutokuwa na uadilifu na usawa katika utendakazi wao. Hao pia kama serikali kuu waweze kuhudumia Wakenya wote na kuchukua hatua bila kujali ni nani analeta hiyo vurugu. Hii ni kwa sababu naamini kwamba serikali iko na uwezo juu ya kila raia. Ndio maana sikubaliani na yale matamshi ya mratibu wa usalama katika Bonde la Ufa aliposema kwamba kuna wahalifu sehemu za Laikipia wako na silaha kushinda silaha za serikali. Kwa hivyo, ni jukumu la serikali kutumia nguvu zake kudhibiti amani na kuhakikisha Wakenya wanaishi kwa amani. Yangu ni hayo kwa serikali kuu. Bw Spika, pia ninawahimiza wenzetu viongozi wakati kama huu wa siasa tuendeshe siasa zetu kwa njia ya nidhamu bila kugonganisha Wakenya. Mara nyingi, Wakenya wanaumia tukiwa tunawaelekeza katika njia mbaya. Ninakushukuru kwa kunipatia fursa hii na kuomba ya kwamba Mwenyezi Mungu atatuweka salama. Mwaka ujao tukifungua Bunge, tuweze kuwa na nguvu ya kuendelea na kazi zetu. Asante."
}