GET /api/v0.1/hansard/entries/1135723/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1135723,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135723/?format=api",
    "text_counter": 262,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Omanga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13175,
        "legal_name": "Millicent Omanga",
        "slug": "millicent-omanga"
    },
    "content": "Bw Spika, asante. Ningependa pia kujiunga na wenzangu kuwapongeza kwa kupitisha bajeti. Kama Maseneta, kweli tumeonyesha kwamba tunaweza kupigania Ugatuzi na kusaidia kaunti zetu kwa changamoto wanazozipitia. Mwaka huu umekuwa wa changamoto nyingi sana. Tumeathiriwa na ugonjwa wa Coronavirus (COVID-19). Umekuwa mwaka mgumu sana kwetu sisi kama viongozi na wananchi wetu ambao tunawaongoza. Watu wengi wamepoteza kazi haswa vijana na akina mama na biashara za watu wengi zimeathiriwa. Tunafunga mwaka na bado nasikia kwamba kama bunge hatujaweza kufanya yanayotosha tuweze kusaidia wananchi wetu kurudi pahali walikuwa kabla ya hii changamoto ya COVID-19. Ningeomba tukirudi mwaka ujao Mungu akitujalia inshallah mwezi wa pili, tuone vile tunaweza kufanya kama viongozi kuwasaidia wananchi wetu warudi kazini na tuweze kuboresha uchumi wetu na wafanyibiashara waweze kurudi kufanya biashara zao."
}